Monday, July 21, 2014

Nilijaribu Kutoa Mimba Ya Ronaldo "Maria Dolores Dos Santos Averiro" Ni Mama Wa Cristiano Aliyasema Hayo Katika Uzinduzi Wa Kitabu Cha Historia Yake.


LISBON, Ureno

Maria Dolores Dos Santos Averiro Mama Yake Ronaldo

Mama yake mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo, amefichua siri kwamba alijaribu kuavya/Kutoa mimba alipokuwa akitarajia kujifungua mwanasoka huyo miaka 29 iliyopita.

Katika kitabu chake kilichozindulia siku za hivi karibuni, Dolores Aveiro anaeleza kuwa daktari wake aliyekuwa akimshughulikia wakati wa ujauzito huo, aligoma kumsaidia katika jitihada zake za kutoa mimba.

Kuona hivyo, Dolores aliamua kuifanya mwenyewe nyumbani alipoanza tabia ya kunywa pombe yenye joto na kisha kushiriki mazoezi makali kupita kiasi akiwa na wazo kwamba hatua hiyo ingepelekea mimba ya Cristiano kucharuka


“Nilitaka kutoa mimba lakini daktari hakuniunga mkono kabisa. Hivyo nilianza kunywa pombe yenye uvuguvugu na kisha kukimbia mpaka pale nilipozirai ila jitihada zote hizo za kutoa ujauzito ule haukufua dafu,” Dolores anaeleza kwenye kitabu hicho cha wasifu wake.

Pamoja na yote mama huyo anakiri kwamba baadaye mwanawe alikuja kubaini ukweli wa mambo na badala ya kuwa na machungu naye, amekuwa akimfanyia utani tu kwa tendo lake hilo ambalo huenda lingemnyima nafasi ya kuwa mwanasoka maarufu zaidi Duniani jinsi alivyo sasa.

“Alipogundua nilichojaribu kufanya, alikuja na kunieleza haya, 'mama hebu tazama, ulitaka kuniavya ila sasa ni mimi ndiye ninayekimu familia nyumbani”. Ronaldo alimwambia mama yake

Mbali Na Hayo 


Kwa wakati huo straika wa zamani wa klabu ya Arsenal na taifa la Ufaransa, Thiery Henry ameibua mjadala ambao umekuwepo kwa siku nyingi wa ni nani mkali zaidi kati ya Lionel Messi na Cristiano.
Wachezaji wote hawa ambao wameshinda mataji ya wachezaji bora duniani Ballon d’Or, Messi anayeisakatia klabu ya Barcelona akiibeba mara nne naye Cristiano akitawazwa mara mbili, wamekuwa wakiwagawanya wadau wengi.
Kulingana na Henry, kando na mambo mengine uwanjani hasa ufungaji mabao, Cristiano hana talanta na kipaji cha kweli kinachoweza kulinganishwa na kile cha Messi.

Cristiano Ronaldo


0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score