Arsen Wenger |
Timu hiyo imeandikisha mwanzo wao mbaya zaidi katika ligi ya EPL tangu 1982 na wamejikuta nyuma mno kwa pengo hilo kubwa la alama ikilinganishwa na muhula uliopita ambapo hadi kufikia wakati huu walikuwa uongozini kabla ya kufifia kufikia mwisho wa kampeni na kunusurika kwa kumaliza wa nne.
“Kuna ushindani mkubwa Uingereza na Chelsea wameanza vyema, hilo tunakubali. Itakuwa vigumu kuwafikia lakini kila mmoja atapigania kuwalaza sisi pia tukiwemo. Huwezi kusema kuwa harakati za kuwania taji zimekwisha baada ya mechi 14 pekee tulizocheza hadi kufikia sasa,” Wenger akasema.
“Hatukuanza vyema msimu huu ila usisahau kwamba hatukuwa na kikosi chote pamoja tangu musimu kuanza kwani ulifuatia Kombe la Dunia. Ni lazima tupambane ili kurudia uwaniaji wa taji kwa haraka katika kila mechi,” akajitetea.
Licha ya yote, Wenger anaonekana kuwa kakalia kuti kavu baada ya mashabiki kuanza kumshurutisha aondoke kama ilivyoshuhudiwa wikendi iliyopita kwenye ushindi wao wa 1-0 dhidi ya West Brom.
0 maoni:
Post a Comment