Thursday, August 29, 2013

AMANI MASHARIKI MWA CONGO BADO NI KITENDAWILI

Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mara ya kwanza kimeshiriki katika mapambano. Hiyo ni hatua inayoelekea katika lengo sahihi
                Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ni sehemu isiyokuwa na utulivu. Mapigano yanatokea mara kwa mara baina ya majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo. Kwa haki kabisa, sasa wakaazi wa eneo la mashariki mwa Kongo wanalitaka jeshi la Umoja wa Mataifa lichukue hatua ili kuyakabili makundi ya waasi.  

Wananchi wataka hatua thabiti:
                                                    Hadi sasa jeshi la Umoja wa Mataifa, Monusco, ambalo ni kubwa kabisa la kulinda amani, kuwahi kuwekwa popote pale duniani, likiwa na askari alfu 19, linakabiliwa na madai ya wananchi wa mashariki mwa Kongo kwamba linashindwa kuutekeleza wajibu wake kwa njia ya ufanisi.
Aghalabu jeshi hilo limekunja mikono nyuma na kutochukua hatua wakati waasi na hata majeshi ya serikali yakifanya vitendo vya kikatili kwa wananchi. Kwa mara ya kwanza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kupitisha azimio namba 2098, mwezi machi mwaka huu, limefungua njia ya kupeleka jeshi lililopewa jukumu madhubuti la kuweza kupambana na waasi.  

Wanajeshi wa serikali watoa silaha kwa waasi: 
                                                                            Jeshi hilo la Umoja wa Mataifa lenye askari alfu 3 kutoka Tanzania, Afrika Kusini na Malawi sasa linapaswa kuthibitisha kwamba, linawalinda wananchi dhidi ya mashambulio ya waasi ambao baadhi yao wanapewa silaha na wanajeshi fisadi wa serikali. Jeshi la Umoja wa Mataifa linapaswa kuyazuia mashambulio ya waasi wakati mwafaka na pia linapswa a kuwanyang'anya silaha waasi hao ili hatimaye kurejesha amani.
Hakika hilo ni jukumu kubwa. Kwani pamajo na waasi wa kitutsi wa M23 wapo wanamgambo wa kihutu wa FDLR, pamoja na wengine kama vile wa Mai Mai Sambamba na harakati za kulinda usalama , jeshi la Umoja wa Mataifa pia linapaswa kuifanya hali ya kibinadamu iwe bora kwa wananchi. Maalfu kwa malfu ya wananchi walivikimbia vijiji vyao katika miezi ya hivi karibuni. Maalfu wanaishi katika mazingira ambayo mwanadamu hastahili katika kambi au wanajaribu kukimbilia misituni, kujificha ili kuwakimbia waasi .

  Askari wa serikali ni tatizo:
                                              Pana tatizo kubwa linalotokana na wanajeshi fisadi wa serikali,waanaobaka na kupora mali za watu.Sasa ni jambo la mashaka iwapo serikali dhaifu ya Rais Kabila itachukua hatua zinasostahili ili kuleta mageuzi katika jeshi la serikali, badala ya kulitegemea jeshi la Umoja wa Mataifa kuyatatua matatizo kwa niaba yake.

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score