Tuesday, January 21, 2014

VIDIC:MAN U KUCHEZA UEFA NI NDOTO

NAHODHA wa Manchester United, Nemanja Vidic, amekiri kwamba hawawezi kutetea ubingwa wao wa ligi kuu msimu huu baada ya
kupokea kichapo cha mabao 3-1 kwa Chelsea.
Beki huyo wa kati aliyeshuhudia wakipoteza mechi yao ya saba ya ligi
kuu Jumapili katika uwanja wa Chelsea Stamford Bridge,alisema kwamba ni muda tu kabla ya Mei ambapo watapokonywa kombe
hilo walilolishinda mara 20.
Aidha mlinzi huyo ambaye alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchuano huo alidokeza kuwepo na uwezekano mkubw awa wa United
kukosa kushiriki UEFA msimu ujao kwani hata kujikatia tiketi kwa kumaliza katika nafsi za nne
za kwanza ligini, utakuwa ni tatizo kwao.
“Nadhani kwa sasa tupo mbali sana kuutetea ubingwa wetu na pengine tuwazie jinsi tunavyoweza kumaliza katika nafasi ya tatu au nne.
Ni suala ambalo sio rahisi kwetu na
itatulazimu kupigana kufa kupona kuhakikisha kuwa tunashiriki shindano la msimu ujao la
klabu bingwa Ulaya,” aliungama.
Matokeo ya wikendi yaliiacha United katika nafasi ya saba ikiwa nyuma ya vinara Arsenal kwa pointi 14. Na licha ya hilo kocha wake David Moyes ana mtazamo tofauti na nahodha wake.
Mkufunzi huyo anayezidi kukumbwa na presha katika klabu hiyo, amekakana kukubali wazo
kuwa kikosi chake hakiwezi kutetea ubingwa huo akishikilia kwamba bado wana nafasi.
“Hatuwezi kufa moyo kwa wakati huu na tutapambana hadi dakika ya mwisho. Majukumu yetu ni kujaribu kumaliza wa kwanza na hilo ndilo tutakalo kuwa tukijaribu kufanya,” Moyes alisema.
Muujiza
Hata hivyo kwa upande wake mkufunzi wa Chelsea, Jose Mouriunho. Mreno huyo anahisi
kwamba kwa United kuhifadhi kombe lao basi watahitaji muujiza wa aina fulani.
“Nina uhakika kuwa David hatakwazika nikimweleza ukweli kwamba wapo nyuma ya Arsenal kwa poiti 14, 13 dhidi ya Manchester City na 12 dhidi yetu. Ikiwa watataka kuhifadhi taji lao, basi pengine itokee kwamba timu tatu zilizoko juu zidorore kwa kiwango kikubwa huku nao wakishinda.
Labda pengine wajizatiti kumaliza wanne kwa sasa,” Mourinho alitoa
mtazamo wake.
MCHIMBA RIZIKI Michezo

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score