Saturday, January 25, 2014

Kesi Ya Kenyatta Utata Mtupu

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Alhamisi (tarehe 23 Januari) iliahirisha kwa muda usiojulikana tarehe ya kuanza kwa kesi uhalifu ya ubinadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyata kutokana na maombi ya waendesha mashitaka.
"Jopo la majaji liliiondosha tarehe ya kuanza kwa kesi ya tarehe 5 Fabruari 2014," ilisema mahakama hiyo kwenye taarifa yake, ikiongeza kwamba kikao kingeitishwa kujadili ombi hilo la upande wa mashitaka.
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, aliomba ahirisho la miezi mitatu la kesi hiyo baada ya kusema mwezi uliopita kwamba hakuwa tena na ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.

Majaji wa ICC walibainisha zaidi kwamba kufuatia ombi hilo la muendesha mashitaka, upande wa utetezi wa Kenyatta ulituma ombi la kufutwa kwa kesi kwa hoja ya kukosekana ushahidi wa kutosha, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.
Bensouda alisema angeweza tu kuendelea na kesi hiyo mara baada ya kuridhika kwamba ushahidi mpya utatosha kuisimamisha kesi hiyo.

Mchimba Riziki

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score