Tuesday, January 21, 2014

Wala Mbwa kutokana na UkameKenya

Kisa cha kusikitisha kimeripotiwa kutokea katika jimbo la Turkana ambapo mwanamke mmoja mkongwe alilazimika kupikia familia
yake nyama ya Mbwa kutokana na uhaba wa chakula unaokumba eneo hilo.
Hali mbaya ya ukame imesababisha uhaba wa chakula na kuwalazimu baadhi ya wakaazi ambao ni wafugaji wa kuhamahama kula nyama ya Mbwa.
Tukio hilo limeripotiwa katika eneo la Kakuma ambapo akina mama wawili walipatikana wakikaanga kitoweo cha nyama ya Mbwa.
Chifu wa eneo hilo Cosmus Nakaya
amethibitishia BBC tukio hilo ambapo, wanawake wawili walikamatwa katika eneo hilo
ambalo ni hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia,wakikaanga kitoweo cha nyama
hiyo tayari kuwalisha watoto.
Mama Akaran Aparo, mwenye umri wa miaka 73, aliambia maafisa kuwa alilazimika kupikia familia yake nyama hiyo kwani hakutaka kuiba Mbuzi au Kuku wa mtu kisha akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Aidha Mama Aparo aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye hulazimika kusafiri umbali wa kilomita 3 kutafuta chakula katika kambi ya Kakuma ingawa hurejea na kidogo sana au wakati mwingine kukosa hata hicho kidogo.
Mama huyo alisema kuwa yeye hutegemea chakula cha msaada kwani anaishi na wajukuu wake watano ambao wazazi wao walifariki.
Anasema yeye hupokea chakula cha msaada lakini hajapokea chochote tangu mwezi Septemba mwaka jana.
Jimbo la Turkana ni kame sana ingawa hivi karibuni kumekuwa na habari njema kutoka katika jimbo hilo kwani visima vya mafuta
vimepatikana pamoja na visima vya maji vilivyo chini ya ardhi.
Utajiri huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wenyeji ingawa hadi mavuno yatakapoanza kupatikana ndipo faida zitakapoanza kudhihirika kwa wenyeji wa jimbo hilo.
Uwezo wa Serikali kutoa msaada wa chakula umekuwa ngumu "alisema mama huyo".
Sitaki wajukuu wangu wateseke "aliendelea kusema mama huyo ajuza ".
Wakati alipokuwa njiani kuelekea katika kambi ya wakimbizi Kakuma, ndipo alipokutana mbwa huyo aliyejenga makazi yake na amezaa watoto watano,ndipo pale aliwachukua watoto wawili wa mbwa huyo kwenda kuwafanya kitoweo.
Kamanda Apiro anasema "mwanamke huyo aliwakata mbwa hao shingo na kuwakaanga kiasili bila kuwachuna ngozi".
Mwanamke nwenzake na mwenye umri kama wake Bi Eregae alisema kwamba "yeye alikuwa ameshindwa kwenda kwenye mahoteli makubwa kutokana na kuthoofika na njaa ".
Aliendelea kusema "mwenzangu aliniita na kuniambia yeye yuko na chakula tunaweza kushiriki"
Shahuda mmoja Peter Lomiyana alisema "aliona mbwa wawili wakikaangwa ndipo akawaita polisi.
"Wakawa wananiuliza kwanini polisi wanatuandama wakati tulisha kula mbwa wawili"alisema afisa wa polisi Samuel Osodo.
Afisa huyo aliendelea kusema msaada wa haraka unahitajika kuwasaidia wanawake hao na watoto walionao.
Chanzo BBC.
MCHIMBA RIZIKI

0 maoni:


Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score