Wananchi wa Kenya wameshangazwa na
taarifa ya mwanamume mmoja aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini
Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji
mkuu Nairobi.
Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa
dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo
kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya
muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa
wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na
hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.
Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu
alikuwa hai.
Source BBC
0 maoni:
Post a Comment