Kiongozi mmoja wa upinzani nchini Zambia,
amekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya
kumchafulia jina Rais wa nchi hiyo Michael
Sata baada ya kumfananisha na Viazi.
Frank Bwalya anadaiwa kumtaja Rais Michael
Sata kama "chumbu mushololwa" kupitia kwa
Redio siku ya Jumatatu.
Katika lugha ya Bemba, tamko hilo lina
maanisha viazi vitamu ambavyo humegeka
vinapopikwa , maana ya ndani ikiwa mtu
ambaye hasikilizi ushauri wa wengine.
Bwana Bwalya anakabiliwa na kifungo cha miaka
mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.
Aidha Bwalya ni kasisi wa zamani na mfuasi wa
zamani wa Rais Sata, ingawa sasa anaongoza
chama cha muungano wa vyama vya upinzani
(Alliance for a Better Zambia (ABZ).
Naibu waziri wa mambo ya ndani, Stephen
Kampyongo alisema kwamba, bwana Bwalya
alikamatwa kwa kutoa matamshi ya kumharibia
sifa Rais Sata.
''Rais Sata ni yule yule aliyekuwa anasikika
kwenye vyombo vya habari akiwachafulia
sifa marais wa zamani, Banda na Mwanawasa
na hakuna aliyemkamata,'' alisema katibu mkuu
wa chama cha ABZ Eric Chanda.
Viongozi wa upinzani wametaka Bwana Bwalya
aachiliwe wakisema kuwa yeye ni mwanasiasa
asiyemuogopa mtu.
'
Waliongeza kuwa matamshi ya Bwalya, "chumbu
mushololwa" hayakuwa matusi.
Mnamo mwezi Sepetamba mwaka jana Nevers
Mumba mwanasiasa mwingine wa upinzani,
alihojiwa na polisi kwa kusema Rais Sata ni
muongo.
S. BBC SWAHILI
MCHIMBA RIZIKI
0 maoni:
Post a Comment