Tuesday, December 31, 2013

BAADA YA OPARESHINI YA TOKOMEZA MAJANGILI KUSITISHWA, VIFO ZA TEMBO VYAONGEZEKA ZAIDI TANZANIA

Kiasi cha tembo 60 wameuawa nchini Tanzania
ndani ya miezi miezi tangu serikali
ilipolazimishwa kusitisha operesheni yenye utata
ya kupambana na ujangili, alisema Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalangu siku ya
Jumapili (tarehe 29 Disemba).

Rais Jakaya Kikwete aliwafukuza kazi mawaziri
wanne mwezi huu kukiwa na tuhuma kwamba
operesheni hiyo ya nchi hiyo dhidi ya ujangili
ilipelekea vikosi vya usalama kufanya matendo
kadhaa yaliyovunja haki za binadamu ikiwemo
kuwauwa washukiwa, mateso na ubakaji.

Lakini Nyalandu alisema angalau operesheni
hiyo ilikuwa imepelekea kupungua kidogo kwa
ujangili. Chini ya operesheni hiyo ya kupambana
na ujangili, vikosi vya usalama vilifanya kazi kwa
sera ya "kupiga risasi na kuua" na kukamata
watu wengi.

"Ndani ya kipindi chote cha operesheni, tembo
wawili tu waliripotiwa kuuawa ambapo sasa
tembo 60 walichinjwa kati ya tarehe 1 Novemba
na 28 Disemba," alisema Nyalandu kwa mujibu
wa shirika la habari la AFP.

Alisema sasa Tanzania itaziomba serikali na
taasisi za mataifa mengine kwa msaada wa
namna gani ya kuendelea nayo.
"Wale watakaoombwa ni pamoja na Umoja wa
Ulaya na nchi za Asia.

Nchi za Asia zinaripotiwa
kuwa watumiaji wakubwa wa pembe za ndovu
na mambo yanatokanayo nazo," alisema
Nyalandu, akiongeza kwamba idara ya
wanyamapori ya Tanzania na shirika la ulinzi wa
wanyama hao vinapaswa kuimarishwa.

Mchimba Riziki

Friday, December 27, 2013

NG'OMBE WA MAAJABU HUKO INDIA, WANAWAKE HUJIFUNGUA WATOTO WA KIUME KILA WAMSHIKAPO NG'OMBE HUYO MWENYE MIGUU MITANO.

Ng'ombe mwenye miguu mitano amekuwa akifanya miujiza nchini India, hii ni kutokana kila mwanamke mwenye mimba akishika mguu huo wa tano hujifungua mtoto wa kiume.

Raj Pratap's ndio jina alilopewa Ngombe  huyo, Raj mwenye miaka mitatu alianza kuonyesha maajabu baada ya mwanamke mwenye watoto wanne kuushika mguu wake watano na mwanamama huyo kujaliwa kupata watoto mapacha  wa kiume kwa mara ya kwanza.

Mwanamama huyo alipojifungua mapacha hao mapema mwezi wa pili mwaka huu,habari hizo zilizambaa kote India kuwa ngombe mwenye miguu mitano mwenye bahati apatikana,kwani katika dini ya Hindu wanaamini kuwa kati ya ngombe 5 millioni lazima mmoja mwenye bahati atapatikana.

Kuanzia siku habari za Ng'ombe mwenye miguu mitano kujulikana, Bwana Pratap amekuwa akijiingizia kipato kikubwa baada ya wanawake 30 kumtembelea Ng'ombe na kuushika mguu huo wa tano ili wapate watoto wa kiume. Bwana Pratap alijipatia  karibia Rupia 500 za India sawa na £5.

Cha kushangaza ni kwamba taarifa zinasema wanawake wote hao waliomshika Ng'ombe huyo waliweza kujifungua watoto wa kiume wote 30.Hii ilisababisha mmiliki wa Ng'ombe huyo kuwa na uhakika hata kukubali kumrudishia mtu pesa kama hatafanikiwa kumpata mtoto wa kiume.

Jumatatu ya 23 Dec mwaka huu, Ngombe huyo alisherekea maajabu yake ya watoto 33 kupatikana baana ya mwanamke aliyeshika mguu wake watano  kujifungua mapacha watatu wote wa kiume.

Bwana Pratap alisema, watoto wote waliokwisha kupatikana ni 33 na wote ni wakiume, mara ya mwisho ni mapacha watatu wamepatikana. Aliongeza "sijui kwanini haya yanatokea  lakini Raju anayo zawadi na ninataka tushiriki na ulimwengu mzima".

Kila siku ninafikiri kumpeleka Raju "Ulaya " ama "Amerika " na kufanya maajabu kule, alisema bwana Pratap.

Katka jamii ya Kihindi watoto wakiume wanapendwa sana kwani wao wanafaida kubwa na ni msaada kwa familia zao.

Mwanamke mmoja aliyepata mtoto wa kiume mwezi wa kumi mwaka huu ambae amekataa jina lake kutajwa amesema,Ni zawadi kutoka kwa Mungu kuushika mguu huu wa tano wa Raju ni bahati sana ,na umenizawadia mtoto wa kiume ninafuha sana.Pia familia yangu wanafuraha sana kwa kujua kuwa niko na kijana.

Ng'ombe wanaabudiwa sana na Wahindi wanaoamini katika dini ya Hindus kuwa Mungu wao Krishna alikuwa ni mchunga ng'ombe. 

Mchimba Riziki

KENYA KUHAMA KUTOKA ANOLOJIA KWENDA DIJITALI VITUO VYA TELEVISION KUFUNGWA.

Kenya ilifunga ishara zote za matangazo ya
analojia saa sita ya usiku wa Alhamisi usiku wa jana (tarehe 26
Desemba) kufuatia uamuzi wa mahakama
mapema wiki hii, The Standard la Kenya liliripoti.

Nation Media Group, Standard Media Group na
Royal Media Services zilizima matangazo yao siku
ya Jumatatu katika kupinga kupuuzwa na
Mahakama Kuu kwa ombi lao la kucheleweshwa
kwa uhamaji kwenda dijitali.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia
Fred Matiang'i alisema kaya nyingi zilikuwa
zimejiandaa kuhamia huko dijitali.

"Kati ya TV zipatazo milioni 1.5 million ndani ya
eneo la awamu yetu ya kwanza kuzima, kiasi cha watu
500,000 tayari zimeshahama kwenda dijitali kwa
sababu wamejiunga na ama DSTV au GoTV,"
alisema. "Hilo linatuacha na kiasi cha watu  milioni na
wale wapatao 700,000 ambao tayari
wameshanunua vigamuzi."

Rufaa ya vikundi vya vyombo vya habari
inatarajiwa kusikilizwa mahakamani siku ya leo
Ijumaa.

Mchimba Riziki

UHURU KENYATTA NA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA HAILEMARIAM DESALEGN WAIZURU SUDAN YA KUSINI KUTAFUTA AMANI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu
wa Ethiopia Hailemariam Desalegn waliwasili
huko Juba Alhamisi hapo jana (tarehe 26 Disemba) kwa ajili
ya mazungumzo na rais wa Sudani Kusini Salva
Kiir yanayolenga kutatua hali ya kukosekana kwa
utulivu kunakoongezeka katika nchi hiyo,Afp iliripoti.

Viongozi hao walipigwa picha kabla ya kuingia
kwenye mazungumzo ya siri.

Ziara hiyo imekuja
katikati ya jitihada zinazoendelea zinazofanywa
na mataifa yenye nguvu ya kanda hiyo kuzuia
hali isiyo na utulivu kwa takribani wiki mbili.

Wajumbe kutoka Kenya na Ethiopia tayari
walishirikishwa katika jitihada za usuluhishi wiki
iliyopita, wakati mawaziri wa mambo ya nje wa
nchi husika walikuwa mojawapo wa ujumbe wa
kanda huko Juba.

Waziri wa nje wa Kenya Amina Mohammed
ameambatana na Kenyatta kwenda Juba, ofisi
yake ilisema.

Kenya imekuwa ikituma ndege kuhamisha raia
wake kutoka Sudani Kusini , ambapo wengi wana
biashara.

Watu elfu kadhaa wanaaminika waliuawa
tangumapambano yalipozuka Sudani ya Kusini ,
baina ya vikosi vinavyomtii Kiir dhidi ya wale
wanaomunga mkono mpinzani wake Riek
Machar, aliyekuwa makamu wa rais ambaye
alifukuzwa mwezi Julai.

Hali ya kukosekana kwa utulivu imechukua sura
ya kikabila, ikilenga kabila la Dinka la Kiir dhidi
ya Nuer la Machar.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga
kura Jumanne kutuma askari wa ziada karibia
6,000 na polisi kwenda Sudani Kusini, karibia
mara mbili ya kikosi cha Misheni ya Umoja wa
Mataifa huko Jamhuri ya Sudani Kusini hadi
vikosi 12,500 na polisi wa kiraia 1,323.

Umoja wa Afrika (AU) na Mamlaka baina ya
serikali za Maendeleo (IGAD) imeelezea kwa
uwazi wasiwasi juu ya kuongezeka kwa vurugu.

"AU na IGAD zimekuwa na wasiwasi mkubwa
kutokana na ripoti ya uhamasishaji wa
wanamgambo wa kikabila huko Sudani Kusini,
jambo ambalo linatishia kuongezeka zaidi kwa
mzozo na kuingia kwenye vurugu baina ya
kikabila zitakazosababisha uharibifu mkubwa
ambazo zingeweza kuhatarisha taifa liliundwa
hivi karibuni la Sudani Kusini," vikundi hivyo
vilisema katika taarifa.

IGAD inatarajia kufanya mkutano wa wakuu wa
nchi kuhusu mzozo wa Sudani Kusini hapa
Nairobi siku ya leo (ijumaa)

By Mchimba Riziki

MWALIMU WA DINI APIGWA RISASI MOMBASA

Ulamaa wa Kiislamu alipigwa risasi na kufariki
dunia na wanaume wenye silaha ambao
hawajafahamika usiku wa Jumatano (tarehe 25
Disemba) huko Ukunda, moja ya eneo muhimu
ya utalii nchini Kenya kandokando ya Bahari ya
Hindi, kusini mwa Mombasa, AFP iliripoti.

"Halikuonekana kuwa tukio la kawaida la
ujambazi," Jack Ekakoro, kamanda wa eneo hilo
alisema Alhamisi.
"Alionekana kuwa mlengwa wa
washambuliaji."

Salim Mwasalim, alivyokuwaa akijulikana
mwalimu huyo wa dini mwenye umri wa miaka
60, "alipigwa risasi wakati akitembea kurudi
nyumbani akitokea kwenye msikiti ulio karibu,"
Ekakoro alisema.

"Tunachunguza kujua sababu na kuwapata
washambuliaji," aliongezea, akisema wauaji
walitoroka kwa pikipiki.

Ulamaa mwingine wa Kiislamu Hassan Mwayuyu
alipigwa risasi kwenye mazingira kama hayo, pia
na wanaume wenye silaha waliokuwa kwenye
pikipiki, katika eneo hilo tarehe 6 Disemba.

Mwasalim alikuwa chini ya uchunguzi wa polisi
katika orodha ya wanaodaiwa kutoa mafunzo
kwa vijana kupambana pamoja na al-Shabaab,
chanzo cha polisi kiliiambia AFP.

By Mchimba Riziki

Wednesday, December 25, 2013

MSIMU HUU WA SIKUKUU ULINZI WAIMARISHWA MARA DUFU KUEPUKANA NA MATUKIO HATARI ZANZIBAR:

MSIMU HUU WA SIKUKUU ULINZI WAIMARISHWA MARA DUFU KUEPUKANA NA MATUKIO HATARI ZANZIBAR:

 Wakati sikukuu ya krismasi inakaribia, ikitoa nafasi ya kuanza kwa kilele cha msimu wa krismasi, polisi wamewaomba wakaazi kuwa waangalifu na kushirikiana na uongozi ili kuhakikisha usalama kwa wote.

"Hali ya sasa ni nzuri, lakini tumeongeza ulinzi katika maeneo yote ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na maeneo ya makanisa," Kamishna wa Polisi wa Zanzibar Hamdan Omar Makame aliwaambia waandishi wa habari. "Tumewaomba viongozi wa makanisa kuripoti kwa polisi nyendo na matukio yoyote wanayoyatilia shaka."

Makame pia alikutana na viongozi wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar katika makao makuu ya polisi siku ya Jumanne (tarehe 24 Desemba) ili kuwahakikishia kuwa polisi wamechukua hatua zote za lazima kuhakikisha usalama wa watalii na raia.

Aliwashukuru kwa kuendeleza ushirikiano wao na viongozi wa usalama na kuomba kwamba wamiliki wa hoteli wote kufunga kamera za usalama katika majengo yao.

"Kila mtu ana jukumu la kutimiza katika kuiweka Zanzibar salama, ikiwa ni pamoja na [kuifanya] mahali salama kwa watalii," alisema.


Matukio ya mashambulizi:
Katika mwaka mmoja na nusu uliopita, mfululizo wa mashambulizi ya tindikali yakiwalenga viongozi wa dini na wageni kutoka nje yaliharibu sifa ya Zanzibar.

Mwezi Novemba 2012, Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga alijeruhiwa katika shambulizi la tindikali wakati akifanya mazoezi ya kukimbia karibu na nyumbani kwake.

Mwaka jana siku ya Krismasi, mtu mwenye silaha alimpiga risasi na kumjeruhi vibaya Padri Ambrose Mkenda, padri wa kikatoliki katika mji wa Zanzibar. Kisha mwezi Februari 2013, mtu asiyejulikana mwenye silaha alimuua padri wa Kikatoliki Evarist Mushi nje ya kanisa lake Zanzibar.

Mapema mwezi Agosti, washambulizi wasiojulikana waliwamwagia tindikali usoni wanawake wawili wa Uingereza wenye umri wa miaka 18 waliokuwa wakiishi Zanzibar na kufanya kazi kama walimu wa kujitolea.

Tarehe 13 Septemba, padri wa Kikatoliki wa Zanzibari Joseph Anselm Mwangamba aliharibiwa sura na washambulizi wasiojulikana ambao walimmwagia tindikali alipokuwa akitoka kwenye mgahawa wa intaneti Mji Mkongwe. Siku kumi baadaye, kundi la washambuliaji wasiojulikana katika gari la pikapu walitupa guruneti kuelekea kwenye eneo lenye maduka mengi katika Mtaa wa Darajani katika mji wa Zanzibar, lakini lilishindwa kulipuka.

Wakristo na Waislamu wa visiwani walio wengi kihistoria wamekuwa wakiishi kwa amani, Makame alisema, hata hivyo uhalifu huo wa kikatili unauchochea umma na kuipa Zanzibar sifa mbaya nchi za nje.

Ili kusaidia kuhakikisha usalama na kuongeza ushirikiano, Makame alisema ofisi yake imekuwa ikihamasisha mikutano na mijadala baina ya dini mbalimbali ili uhusiano mzuri kati ya Waislamu na Wakristo uimarishwe.

Wakristo wanafikia asilimia 3 ya watu milioni 1.2 wa Zanzibar, walio wengi kati ya hao ni Waislamu.


Wajibu wa Uamsho wachunguzwa:
Bado haieleweki kama mashambulizi ya tindikali na matukio mengine yanachochewa kidini, lakini vurugu za hapa na pale zilianza baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid Hadi Ahmed mwezi Oktoba 2012.

Uamsho, ulitokana na shirika la hisani la dini kuwa chama cha waliojitenga wakidai uhuru kutoka Tanzania.

Ahmed ana viongozi wengine tisa wa Uamsho bado wanashikiliwa, wakishtakiwa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kuchochea vurugu na fujo, na njama za kuhatarisha amani na utulivu, miongoni mwa makosa mengine. Walikuwa hawajashitakiwa na walikataliwa dhamana chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa. Walikuwa wanasubiri rufaa katika Mhakama Kuu ili kubatilisha uamuzi wa dhamana.

Viongozi wa Uamsho na wafuasi mara kwa mara wamekuwa wakileta wasiwasi wa kidini katika visiwa, lakini taasisi wakati wote imekuwa ikikanusha kuhusika.

Katika mikusanyiko kadhaa mwaka jana, viongozi wa Uamsho walitetea uhuru wa Zanzibar kutoka katika muungano wa sasa na Tanzania ili kutekeleza sheria za Kiislamu.

"Viongozi wa Uamsho wanaamini kwamba uhuru wa Zanzibar utasaidia kutunza utamaduni wa Kiislamu ambao umeharibiwa na mwingiliano wa mtindo wa maisha wa kigeni unaoletwa na wageni na kuigwa na vijana wa nchini," Ahmed aliwaambia waliohudhuria katika mkusanyiko kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Lumumba mwezi Mei 2012.

Hassan Khatib, mwenye umro wa miaka 32, mwalimu katika shule ya dini na mfuasi wa Uamsho anayeishi Zanzibar, alisisitiza kusema kauli yake na kupuuza tuhuma kwamba kikundi kinachochea vurugu.

"Tunataka nguo za heshima hatutaki sketi fupi," Khatib aliwambia waandishi wa habari. "Tunapinga kuongezeka kwa baa, na tunadai uhuru wa Zanzibar ili tuweze kujenga uchumi wetu na kulinda utamaduni wetu."


Vurugu zatishia tasnia muhimu ya utalii:
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Saidi Ali Mbarouk alisema kwamba mwaka jana tasnia ya utalii, ambayo inachangia asilimia 27 ya pato ghafi la ndani la Zanzibar, iliathiriwa vibaya sana na vurugu.

Tasnia inaajiri moja kwa moja watu 15,000, wakati zaidi ya kazi nyingine 35,000 zinatokana moja kwa moja na utalii, alisema.

"Machafuko yaliyochochewa na kikundi cha Uamsho cha Waislamu mwezi Oktoba mwaka jana, yakifuatiwa na mashambulizi ya viongozi wa dini yameharibu sifa ya Zanzibar," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba kutokuwa na utulivu kumesababisha kushuka kwa utalii, ambako serikali inajaribu kuzuia katika msimu mkuu wa mwaka huu.

Kipindi cha watalii wengi Zanzibar ni kuanzia katikati ya mwezi Juni hadi Septemba na katikati ya Desemba na Februari.

Kutokana na hatua za kukinga zilizochukuliwa kuhakikisha usalama, Mbarouk alisema mamlaka zilikuwa zikitarajia kila kitu kuendeshwa kwa amani kuzunguka katika maeneo ya utalii wakati wa sikukuu.

"Hatutarajii tukio lolote wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya," alisema. "Tunawaomba wananchi kuwakaribisha wageni."

Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar Abdulsamad Ahmed Saidi alikiri kwamba hadi sasa mambo yanaonekana kuwa mazuri.

"Utafiti tulioufanya wiki iliyopita unaonyesha kwamba kuna uthabiti wa biashara katika utalii na ushikaji mzuri wa nafasi kwani katika baadhi ya hoteli nafasi zimejaa," aliwaambia waandishi wa habari.

"Tumelalamika kuhusu usalama, lakini serikali ilijibu vizuri kwa kuongeza maofisa usalama zaidi na pia kuhamasisha polisi jamii, hususani kuzunguka maeneo ya vivutio vya utalii kama vile Mji Mkongwe wa Zanzibar," alisema Saidi.


Hofu inaendelea kuwa kubwa:
Pamoja na uhakika kutoka kwa viongozi wa serikali, hofu inaendelea kuwa kubwa miongoni mwa jamii ya Kikristo.

"Tuko imara na tunaamini yote yataendelea vizuri, lakini jamii ya Kikristo ina wasiwasi," alisema Michael Hafidh, mhubiri katika Kanisa la Anglikani la Zanzibar. "Tumekuwa tukiishi [pamoja] kwa amani kwa miaka mingi, lakini baadhi ya watu wanatugawanya."

Aliwaomba polisi kuendelea kufanya jitihada za kuwasaka watu wanaosababisha hofu na wasiwasi wa kidini visiwani hapo.

Dickson Kaganga, askofu wa Kanisa la Assemblies of God huko Zanzibar, mojawapo kati ya makanisa yaliyolengwa wakati wa maandamano mwaka jana, alisema waumini wake walikuwa na wasiwasi lakini wana matumaini.

"Wote tuna haki ya kushiriki katika dini zetu huko Zanzibar," aliwaaambia waandishi wa habari, akitoa wito kwa polisi kuhakikisha kila mmoja anakuwa salama.

Sheikh Soraga pia alitoa wito wa waamini kuwa na uvumilivu na kushirikiana kwa amani huko Zanzibar, akisema kisiwa hakiwezi kuendelea kama hali ya wasiwasi wa kidini na kisiasa iliopo sasa itaendelea.

"Tuepuke migogoro isiyo ya lazima. Kuna baadhi ya watu wenye ndoto za kisiasa, wanatumia dini kuligawa taifa.

Mchimba Riziki
Tunakutakia X-Mass Njema Na Heri Kwa Mwaka Mpya.

Sunday, December 22, 2013

HAWAJALI GHARAMA KUBWA ZA SMARTPHONE BALI WANACHOJALI NI MAWASILIANO

Licha ya gharama kubwa za awali za kununua smartphone, Wasomali wanaongezeka katika kulipia kutokana na faida za kuunganishwa papo hapo na intaneti, kunakorahisisha mawasiliano na wanafamilia walio nje ya nchi na kupata habari na taarifa kwa urahisi na kwa gharama nafuu kuliko njia iliyokuwa imezoeleka ya kupata intaneti.

"iPhones ya gharama kubwa kabisa ni dola 800, wakati [simu] Samsung ziliuzwa kwa dola 500, ingawaje zipo baadhi ambazo zinagharimu zaidi," alisema Faisal Abdullahi mwenye umri wa miaka 34 ambaye anamiliki duka la kuuza simu za mkononi katika soko la Hamar Weyne huko Mogadishu. Smartphone ya gharama ndogo kabisa iliuzwa kwa dola 250, alisema.

Uuzaji wa smartphone umeongezeka kwa haraka, Abdullahi alisema, akinukuu kwamba duka lake liliuza smartphone 12 mwaka 2012, na takriban 100 mwaka huu.

Abdullahi alisema wateja wake wengi wanaulizia smartphone, hususani simu za mkono za Samsung, ambazo zinafahamika sana kwa sababu ni bei rahisi kuliko iPhone na zina programu za bure zaidi.

"Baadhi ya simu hizi ni ghali sana ingawaje kwa sasa zinauzwa kwa gharama nafuu kidogo kuliko zilipokuja kwa mara ya kwanza ," alisema. "Unaweza kuona nyingine ni ghali sana, lakini tunaziuza kila mara."

Gharama ndogo za matumizi ya data:

Abdisalam Warsame, mwenye miaka 20 mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Djibouti katika wilaya ya Wadajir, alisema alimshukuru dada yake aliyeko Saudi Arabia ambaye alimtumia fedha kununua smartphone miezi nne iliyopita.

"Nilizoea kwenda katika mgahawa wa intaneti ambao unatoza shilingi 18,000 za Somalia kwa saa wakati nilipohitaji kutumia intaneti, na inawezekana kuihitaji mara kadhaa kwa siku,. "Sasa ninalipa dola 1 (shilingi 20,000) kwa zaidi ya saa 24 katika smartphone yangu."

Kwa upatikanaji wa intaneti katika simu yake ya mkononi, Warsame alisema sasa anaweza kuwasiliana na nchi nyingine duniani wakati wote.

Vivyo hivyo, mkaazi wa Mogadishu mwenye miaka 32 Yusuf Ibrahim alisema amekuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa intaneti katika simu ya mkononi kwa miezi mitano iliyopita.

Alisema huduma hii imefanya iwe rahisi kwake kuendelea kuwasiliana na wanafamilia wake wanaoishi Finland.

"Ninawasiliana na mke wangu na watoto katika WhatsApp kila siku," Ibrahim alisema . "[Ninahisi] kama vile niko pamoja na wao, na ni nafuu kuliko kuongea nao moja kwa moja. Nilikuwa nalipa zaidi ya dola 50 hapo kabla kuongea nao tu, lakini sasa ninatumia chini ya dola 10 kwa mwezi, ingawa nawasiliana nao kila saa."

Abdirashid Hussein mwenye umri wa miaka 35, mfanyakazi wa kampuni ya intaneti na simu za mkononi ya Hormuud Telecom, alisema 1 gigabyte (GB) ya data ya intaneti inagharimu dola 25, na muda itakayodumu inategemea matumizi ya mtu.

Licha ya Hormuud, Somtel iliyoko Hargeisa ni kampuni nyingine pekee inayotoa huduma ya intaneti kupitia simu za mkononi huko kusini mwa Somalia.

Aweys Abdirahman, mwenye umri wa miaka 23 mwanafunzi katika Shule ya al-Imra katika wilaya ya Hodan Mogadishu, alisema simu za kisasa zinarahisisha kwa Wasomali kuwa wameunganishwa, ingawaje wakosoaji wanasema kwamba vijana wanatumia muda wao mwingi kwenye smartphone zao.

Somalia iko nyuma sana katika suala la upatikanaji wa intaneti, hata hivyo, ongezeko la matumizi ya intaneti ya simu ya mkononi ya gharama nafuu inasaidia kuziba pengo mwaka baada ya mwaka, alisema.

"Kwa upande mmoja sio ghali sana kwa sababu kiasi cha fedha ninachotumia kupata intaneti sasa ni [chini ya] kile nilichokuwa nikitumia kwa kupiga simu [pekee yake]," alisema Abdirahman, akiongeza kwamba anahifadhi fedha kwa kutuma ujumbe mfupi kwa marafiki zake na familia badala ya kupiga simu.

Faisal Muse Mohamed, mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 24 anayefanya kazi katika Redio Mogadishu, amekuwa akipata intaneti kupitia smartphone yake kwa mwaka sasa.

Hususan, anasema anatumia simu yake ya aina ya Samsung Galaxy kupata mitandao ya kijamii kama vile Facebook, ambako huingia kuwasiliana na kupata habari.

"Ninatumia Facebook zaidi kwa sababu unaweza kuwasiliana na marafiki na kupata taarifa na picha zinazokwenda na wakati ambazo zimetumwa," . Alisema anatumia pia Whatsapp kuwasiliana na marafiki kwa sababu sio gharama kubwa na haihitaji matumizi makubwa ya data.




Kuchukua nafasi ya mikahawa ya intaneti
Hassan Mohamed, mkazi wa Mogadishu mwenye umri wa miaka 30 ambaye anasoma sosholojia katika Chuo Kikuu cha Somalia, alisema smartphone ni njia binafsi zaidi ya kupata intaneti, kuunganishwa na watu na kuwa na taarifa wakati wote.

"Sasa ninajisikia kwamba nina uwezo wa kupata intaneti wakati wote ninapoihitaji badala ya kuwategemea [watoa huduma wengine] wa intaneti kama zamani," alisema Mohamed, ambaye amekuwa akitumia simu aina ya Samsung Galaxy kwa karibia miezi saba sasa.

"Ninaitumia kutuma baruapepe, kupata taarifa kuhusu habari, na pia ninatumia kupata tarifa zinazohusiana na masomo na taarifa kutoka katika Google na kupata mitandao ya kijamii," .
"Ninaweza pia kusoma au kutazama chochote ambacho ni faragha kivyangu. Kwa kuwa maeneo ya huduma za intaneti ni maeneo ya umma, huwezi kupata au kutazama kila kitu unachokitaka," alisema.


Mchimba Riziki

Tuesday, December 10, 2013

Tanzania Yaadhimisha siku Ya Uhuru: Vita Kubwa Yatangazwa.

Tanzania yaadhimisha
siku ya uhuru huku
kukiwa na miito ya vita
kubwa zaidi dhidi ya
umasikini:

Tanzania iliadhimisha miaka 52 ya uhuru wake
siku ya Jumatatu (tarehe 9 Disemba) lakini
wasomi wengi wameikosoa serikali kwa
kutokufanya jitahada za kutosha katika kuondoa
umasikini miongoni mwa raia.

Kwa mujibu wa Honest Ngowi, profesa wa
uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe, pato
la jumla la Tanzania linakua kwa asilimia 7 kwa
mwaka, lakini hali ya uchumi kwa Watanzania
wengi inazorota.

"Tunapaswa kuhakikisha ukuaji wa uchumi wetu
unapunguza umasikini wa watu, na hasa
Watanzania wa kawaida,"

Aliongeza kwamba Tanzania ina uhuru wa
kisiasa lakini si uhuru wa kiuchumi, ambao ni
muhimu kwa maendeleo ya kijamii

Gaudence Mpangala, profesa wa sayansi ya
siasa kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
alikubaliana na hoja hiyo.

Alisema kwamba takwimu ambazo
Tanzania inaonesha kwa washirika na wafadhili
wa kimataifa zinaonesha kwamba uchumi wa
nchi hiyo unakuwa kwa kasi, lakini kiuhalisia
wananchi masikini hawaoni manufaa yake.

Benson Banna, profesa wa sayansi ya jamii
kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliisifu
serikali kwa kudumisha amani na utulivu ndani
ya miaka 52 iliyopita, lakini uwekezaji zaidi
unahitajika kwenye elimu na viongozi lazima
wabadilike kutoka kuwa wapangaji na kuwa
watekelezaji.

"Viongozi wetu wanaongea sana," Bana aliiambia Chanzo cha habari.

"Wakati umefika sasa kwa viongozi wetu wawe
watu wa vitendo zaidi badala ya kupiga soga.

Hii ndiyo njia pekee ya kufikia maendeleo
yanayoonekana kwa nchi yetu."

Tanzania ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza
tarehe 9 Disemba 1961.
Wakati huo huo, Benki ya Dunia ilikubali
kuendelea upya na msaada wake kwa Mfuko wa
Jamii wa Tanzania (TASAF) baada ya kutathmini
vyema maendeleo yake ya siku za karibuni chini
ya mpango wa TASAF-III, liliripoti gazeti la Daily
News la Tanzania.

"Benki ya Dunia itaendelea kuisadia serikali ya
Tanzania katika kuhakikisha malengo ya kuondoa
umasikini yanafikiwa," alisema afisa wa Benki ya
Dunia Denny Kalyalya wakati wa ziara yake
kwenye kijiji cha Fukayosi siku ya Jumamosi
(tarehe 7 Disemba).

Mchimba Riziki.

Friday, November 29, 2013

Dini Isiyoamini Dawa Yeyote Iliyotengenezwa Na Mwanadamu, wanaamini Maombi Ya Dini Yao, Fuatili Hapa Ndani

TANGU 1977, Mzee Kavulu Musembi hajawahi
kutumia dawa ama hata kushika dawa na
mikono yake japo amekuwa akiugua mara kwa
mara.
Hii ni kwa sababu ya imani yake kuwa
Mungu ndiye mponyaji pekee na hana imani na
vitu vilivyotengenezwa na binadamu kama vile
dawa.

Mzee Kavulu ni mmoja wa waumini wenye imani
kali wa dhehebu la Kavonokya katika eneo la
Mwingi, Kaunti ya Kitui.
Bw Kavulu, ambaye
alijiunga na Kavonokya
akiwa kijana wa umri
mdogo mnamo 1976,
anasema kulemewa na
ugojwa ndio kulimfanya
ajiunge na dhehebu hilo.

“Nilipatwa na ugonjwa
mbaya na nikapelekwa na ndugu yangu Nairobi
kupata matibabu.
Nililazwa hospitalini kwa wiki
kadha bila nafuu yoyote na wakati mmoja
nikaona maisha yangu yamefika mwisho.

Baada
ya kurudi nyumbani nilifanyiwa maombi na
waumini wa Kavonokya na nikapona kabisa,”
alieleza Mzee Musembi.

Wazazi wa Mzee Musembi walikuwa wanaamini
tamaduni za jamii ya Wakamba hivyo alikuwa
wa kwanza katika familia yao kujiunga na
dhehebu hilo.

“Sijawahi kupeleka watoto wangu sita hospitalini
tangu wazaliwe na sasa ni watu wazima na
baadhi yao wana shahada za digrii kutoka vyuo
vikuu,” alisema.

Alisema watoto wake wote walizaliwa nyumbani
na hawajawahi kupata chanjo hata moja hata
baada ya kuugua ukambi.

Kwa miaka mingi wafuasi wa dhehebu la
Kavonokya wamekuwa wakikabiliwa na utata
kuhusu imani yao ya kususia matibabu kwa
madai kuwa wanaamini uponyaji hutoka kwa
Mungu pekee na wala si kutokana na matibabu
ya hospitalini.

Baadhi ya vijiji katika wilaya ya Mwingi Mashariki
vimedhibitiwa na waumini wa Kavonokya ambao
wanakutana kila siku ya Jumapili sawa tu na
Wakristo wengine kwa ibada.

Waumini wa dhehebu la Kavonokya mara kadha
wamegonga vichwa vya habari katika mzozo wao
na maafisa wa afya wakitakiwa kupeleka watoto
wao kupata chanjo.

Bw John Kasembei ambaye ni mfuasi wa
dhehebu hilo kutoka eneo la Mwingi anaeleza
kuwa walioanzisha vuguvugu hilo miaka ya
hamsini walikuwa na ushuhuda wa pamoja wa
jinsi Mungu alivyowaponya kutokana na maradhi
tofauti tofauti ambavyo binadamu hangeweza.

“Ni kutokana na neno la Kikamba 'vonokya’
kumaanisha kuokolewa ambapo walitoa jina
'kavonokya’,” anasema Bw Kasembei.

Wafuasi wa dhehebu hili hutambulika kwa imani
yao kali ambayo wanasema inawatofautisha na
waumini wa madhehebu mengine.

“Mimi
nimejaribu kuwa muumini wa makanisa
mengine lakini ni katika dhehebu la Kavonokya
ambapo kuna imani ya kweli.

Hautawahi kusikia
waumini wetu wakiwa na mizozo kama
makanisa haya mengine,” alielezea Bw
Musembi.

Waumini wanawake wa Kavonokya hutambulika
kwa marinda yao marefu na kujifunga vitambaa
kichwani.
Mavazi yao yanafanana na yale ya wafuasi wa
dhehebu la Akorino lakini wanaume hawajifungi
vitambaa kichwani.

Bw Kasembei anaeleza kuwa mavazi yao
yanatokana na mafunzo ya Biblia kuwa
mwanamke afunike kichwa chake haswa wakati
wa ibada.
“Kulingana na kitabu cha Wakorintho
wa kwanza katika mlango wa 11, Biblia imeeleza
mwanaume ndiye kichwa cha jamii na hivyo
kutaja jinsi kichwa cha mke kinafaa kunyolewa
au kufunikwa kama ishara ya unyenyekevu,”
alielezea.

Marinda yao marefu yaliyo na mikunjo ni
kuhakikisha kuwa mwanamke anaficha uchi
wake na havai rinda linaloonyesha umbo lake
hata wakati wa upepo, rinda hilo linamsitiri
vilivyo.

Wakati kunapozuka maradhi ya watoto haswa
ugonjwa wa kupooza na ukambi inawalazimu
maafisa wa afya kwa ushirikiano na maafisa wa
usalama na viongozi wa eneo hilo kuwashinikiza
kwa lazima waumini wa dhehebu hilo
kuwapeleka watoto chanjoni.

Chifu wa wa eneo hilo la Endui katika wilaya ya
Mwingi ya Kati, Bw Samuel Maithya anasema
mara nyingi inambidi kuwachukua watoto
wanaougua kwa lazima na kuwapeleka kupata
matibabu.

“Mwaka jana watoto kadhaa ambao wazazi wao
ni wafuasi wa kavonokya walipoteza maisha yao
wakati ugonjwa wa ukambi ulipochipuka katika
eneo hili,” asema Bw Maithya.

Waumini hao huamini kuwa imani yao huponya
hata magonjwa yasiyokuwa na tiba ya
kimatibabu.

“Hakuna pahali katika Biblia ambapo Wakristo
walienda hospitalini. Walikuwa wakiponywa na
Yesu mwenyewe au katika maziwa kama lile la
Bethsaida ambapo malaika alikuwa akishuka na
kukoroga maji ili mgonjwa wa kwanza kuingia
majini apone,” alielezea Bw Musembi.

Kulingana na mafunzo ya dhehebu hili, watu
hupata magonjwa kwa sababu ya mambo
matatu:
Majaribu ya kupima imani ya Mkristo,
njia ya Mungu kuadhibu Mkristo kwa maovu
yake au njia moja ya Mungu kumpumzisha mtu
kama siku zake za kuishi zimeisha duniani.

Waumini hawa huamini kuwa dawa si mwisho
wa magonjwa duniani na kuwa cha muhimu ni
mtu kuwa na imani na kupata uponyaji wa bure
kutoka kwa Mungu.

“Iwapo ni kweli matibabu
ya dawa yanaweza kuponya magonjwa, ni kwa
nini hospitali huwa na vyumba vya kuhifadhi
maiti?,” alishangaa muumini mmoja.

Wafuasi hawa wanasema watashikilia imani yao
hata serikali ikiamuru watoto wapewe chanjo.

Wanaamini kuwa siku ya mtu kufariki ifikapo,
hata dawa zinazoaminika kuwa bora zaidi
haziwezi kuzuia kifo.

Bw Kasembei anasema kuwa ugonjwa wa
Ukimwi ni dhibitisho kamili kuwa mwanadamu
hawezi kutengeneza dawa za kuponya magonjwa
yote.

“Wagonjwa wa Ukimwi humlilia Mungu
awaponye kwani hata dawa za kupunguza
makali yake haziwezi kuponya ugonjwa huo,”
akasema.

Anasema wao hutambua magonjwa kama pepo
mbaya inayowajia wanadamu na kuwa dawa ni
vitu vilivyotengenezwa na wanadamu kutumia
akili yao na si kitu kitakatifu mbele ya Mwenyezi
Mungu.

Waumiwa hao walisema kuwa idadi
ya watoto wao wanaofariki kutokana na
michipuko ya maradhi kama ukambi ni ndogo
mno ikilinganishwa na ile ya watoto wanaopona
baada ya kufanyiwa maombi katika dhehebu
hilo.

Bw Kasembei amekuwa katika kazi hii ya
kuhubiri sehemu mbalimbali na anasema kuna
wafuasi katika maeneo mengine nchini.

“Nimehubiri na kubatiza watu katika mji wa
Eldoret, Nairobi, Kati, Eldama Ravine, Busia,
Marachi, Ahero na Kisii ambapo wote huamini
Kavonokya.”

Ibada

Kavonokya hukutana siku ya Jumapili kwa ibada
yao sawa tu na Wakristo wengine duniani.

Wafuasi hawa hutumia Biblia ya kawaida
inayosomwa na Wakristo wengine.

Maombi
hufanywa kwa pamoja huku kila mmoja akiwa
amepiga magoti.

Cha kushangaza ni kuwa waumini hawa
hawafanyii ibada zao katika makanisa. Wao
hukutana katika boma za washirika wao.

Waumini hawa wanasema hatua ya kutokuwa na
makanisa ni kwa sababu hawataki washirika
wake kutumia pesa zao kwa ujenzi wa makanisa.
Wanaamini kwamba kanisa ni roho ya mtu.

Wakati wa ibada wanawake na wanaume
hawatangamani kwani kila jinsia inakaa upande
wake. Vilevile wanawake hawakubaliwi kuongea
au kutoa mafunzo yoyote wakati wa ibada.

Masomo yote ya Biblia pamoja na mahubiri
hufanywa na wanaume pekee. Wakati wa
kuimba pekee ndio wanawake wanakubaliwa
kusimama na kuimba kwa pamoja na pia wakati
wa maombi.

Jambo hili la wanawake kukaa kimya wanasema
ni kulingana na kitabu cha Wakorintho wa pili
mlango wa 14 ambapo wanawake wanatakiwa
kukaa kimya na kuacha wanaume kuongoza
ibada.

Dhehebu hili halina wahubiri au kiongozi yeyote,
kila mfuasi wa kiume ana uhuru wa kuhubiri
neno alilopewa na Mungu.

Sherehe za ndoa huongozwa na mwanaume
yeyote aliyekomaa miongoni mwa waumini hao.
Kinyume na Wakristo wengine duniani , waumini
wa Kavonokya hawavalishani pete wakati wa
harusi na vilevile hakuna cheti chochote cha
harusi kwa wanaooana.

Wanasema pete na vyeti hivyo hutolewa na
madhehebu yale ambao yamejaa unafiki wa
kukubali talaka miongoni mwa waliooana.

“Hatuhitaji pete au cheti chochote kwani Mungu
ndiye shahidi mkuu wala hatuna hofu ya watu
kutengana baada ya kuoana,” akasema muumini
mmoja.

Waumini hawa pia hawatumii vitabu vya nyimbo
wakati wa ibada na huimba kwa pamoja bila
mtu yeyote kuongoza.
Vilevile wafuasi hawa huimba bila ala za muziki
zozote na hucheza kwa kuruka juu huku
wakipiga makofi.

Hawatoi sadaka yoyote wakati wa ibada au hata
kutoa fungu la kumi. Wanaamini kuwa hakuna
haja ya kumtolea Mungu asilimia kumi huku
mtu akibaki na asilimia tisini kwa matumizi yake
binafsi. Badala yake wao hutumia asilimia
kumi na kutenga asilimia tisini kwa kazi ya
kuhubiri neno la Mungu, kusaidia maskini na
watoto yatima.

Bi Nzakya Mutava ni muumini wa Kavonokya
anayeishi katika eneo la Mwingi. Anasema
alikuwa na shida ya kuzaa watoto na kufariki
wakiwa na umri mdogo bila kuugua.

Bi Nzakya
anasema alipoteza watoto wanne katika hali hiyo
na kuamua kuomba na wafuasi wenzake kabla
ya kupata mimba ya mtoto wa tano.
“Tuliomba kwa muda mrefu hata wakati
nilipokuwa na mimba ya mwanangu wa tano na
alipozaliwa tukazidi kuomba, hivi sasa nina
watoto wanane na wote wana afya njema,”
akasema.

Bi Mwalale Ngui anasema hapo mwanzoni
hakutaka kuhusishwa na dhehebu la Kavonokya
kwani hakuamini mwanadamu angeishi bila
kupata matibabu hospitalini.

Mambo yalimgeukia alipougua maradhi ambayo
hayakuweza kutambuliwa na madaktari.

“Nilitumia mali yangu yote nikijaribu kupata
uponyaji hadi nilipoishiwa ndipo niliamua
kujiunga na Kavonokya,” akasema.

Mchimba Riziki

MWANAUME AVUMANIWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NA MBUZI NI HUKO MALINDI:


Mwanamume wa miaka 20 amepigwa na
kujeruhiwa vibaya na wananchi baada ya
kufumaniwa akishiriki kitendo cha ngono na
mbuzi kijijini Dabasom lokesheni ya Watamu
wilayani malindi.

MWANAMUME wa miaka 20 Alhamisi alipigwa na
kujeruhiwa vibaya na wananchi baada ya
kufumaniwa akishiriki kitendo cha ngonona
mbuzi kijijini Dabasom lokesheni ya Watamu
wilayani malindi.

Moses Katana alionekana na mwenye
mbuzi huyo ambaye alipiga mayowe
yaliyowavutia wanakijiji waliomkabili mshukiwa.

Baada ya kutandikwa vya
kutosha, mshukiwa
alikokotwa hadi ofisini
kwa chifu wa Dabaso Bw
Joseph Baya Maitha,
ambapo chifu aliwataka
maafisa wake wa polisi
wa utawala waingilie kati
na kumwokoa mshukiwa
aliyekuwa akiendelea kurushiwa makonde.

Baadaye mwanamume huyo alipelekwa katika
makao makuu ya polisi mjini Malindi na
kufunguliwa mashtaka ya kufanya kitendo cha
ngono na mnyama.

Chifu Baya alisema kwamba visa vya vijana
kupatikana wakishiriki vitendo vya ngono na
wanyama vimekuwa vikiongezeka mno katika
eneo hilo, na akawatahadharisha kwamba
watakabiliwa na mkono wa sheria iwapo
watapatikana.

Msomaji wangu kwa hayo yote nakuomba jaribu kuyapitia maandiko ya Mungu ili uweze kuyakemea mapepo kama haya.

Kumbukumbu La Torati 27:21 ama soma Kumbukumbu la Torati yote 27.

Mchimba Riziki

Thursday, November 28, 2013

Makaburi Yafukuliwa Na Maiti Waliokuwemo Kuibwa Huko Kakamega.

Wakazi katika kijiji kimoja cha Kaunti ya
Kakamega, jana asubuhi walipigwa na mshangao
baada ya watu wasiojulikana kufukua makaburi
mawili na kuiba maiti.

WAKAZI katika kijiji kimoja cha Kaunti ya
Kakamega, Jumanne asubuhi walipigwa na
mshangao baada ya watu wasiojulikana kufukua
makaburi mawili na kuiba maiti.
Wanakijiji cha Shirere walisema makaburi hayo
ni ya watu wawili wazaliwa wa Ulaya waliozikwa
mahali hapo yapata miaka 70 iliyopita.

Makaburi hayo, ambayo
yamo kwenye uwanja
wazi karibu na Shule ya
Upili ya Bishop Sulumeti
yalikuwa yametelekezwa
kwa muda mrefu.

Mzee wa kijiji, Bw Andrew
Andanyi alisema mmoja
wa watu waliozikwa mahali hapo alikuwa rubani
aliyekufa kwenye ajali ya ndege.

“Makaburi haya
yamekuwepo tangu 1940 nilipokuwa mvulana,”
alisema.

Wanakijiji walisema watu wawili wasiojulikana
walitembelea mahali hapo siku mbili kabla ya
tukio hilo.

Wezi hao waliacha chupa tupu za pombe, ishara
kwamba walikunywa pombe kabla ya kufukua
maiti hizo.

Naibu wa chifu wa sehemu hiyo, Bw Morris
Mukabane alisema tukio hilo linaendelea
kuchunguzwa.

Kwingineko, vijana waliokodishwa walifukua
maiti ya mfanyabiashara wa Nakuru ambaye
mkewe na wazazi wake wanazozania mahala
atakapozikwa.

Maiti ya Evans Bari Omuhindi ambayo ilikuwa
imezikwa kwenye makaburi ya Nakuru North
dhidi ya matakwa ya wazazi wake, ilifukuliwa
Jumatatu jioni kufuatia amri ya mahakama.

Mwanaume huyo aliyeaga dunia Novemba 1
alizikwa na mkewe Bi Jesica Kanyi lakini wazazi
wa mwenda zake na mwanamke anayedai kuwa
mkewe wa pili walienda kortini kupinga hatua
hiyo.

Watoto watatu
Walidai kwamba mwili wa marehemu ulifaa
kuzikwa katika kijiji cha Ebuskami Emanake,
nyumbani alikozaliwa katika eneo la Luanda
kulingana na mila za Waluhya.

Mamake marehemu Bi Sofia Nekesa alisema
hata kama mwanawe alikuwa akiishi mjini
Nakuru na mkewe wa kwanza na watoto wao
watatu, alikuwa pia amemuoa Bi Dinah Saisi na
wakapata naye mtoto mmoja.
Bi Saisi alikuwa
akiishi na wa wazazi wa marehemu eneo la
Luanda.

Jumanne, afisa anayesimamia kituo cha polisi
cha Nakuru Central alimwambia Hakimu Mkazi
wa Nakuru, Bi Victoria Ochanda kwamba polisi
walikuwa wameufukua mwili kama korti
ilivyoagiza.

Alisema mabaki hayo yalipelekwa kwenye
chumba cha maiti cha Manispaa ya Nakuru
ukingoja uamuzi wa korti.

Chanzo Taifa Leo

Shared by,

Mchimba Riziki.

Uganda yateua naibu mpya wa kamanda wa kikosi cha AMISOM

Meja Jenerali Geoffrey Baraba Maheesi wa
Uganda, ambaye ameteuliwa kuwa naibu
kamanda wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini
Somalia (AMISOM), aliwasili nchini Somalia
Jumanne usiku (tarehe 26 Novemba), gazeti la
Daily Monitor la Uganda liliripoti.

Muheesi amechukua nafasi hiyo katika kipindi
ambacho wanajeshi 24 wa Uganda
walisimamishwa kwa muda mwezi Septemba
kwa kutuhumiwa kuuza chakula kilichokusudiwa
kwa ajili ya wanajeshi wa AMISOM .

Kamanda wa
kikosi cha Uganda Brigadia Michael Ondoga
alikuwa miongoni mwa wale waliosimamishwa.

"Nitapambana kwa kila hali kurejesha utu wa
[Jeshi la Ulinzi la Watu wa Uganda] nchini
Somalia, makosa yamefanywa lakini
tutayarekebisha," alisema Maheesi.

"Ninajua kazi inayotukabili ni ngumu lakini rekodi
za ufuatiliaji wangu ziko wazi na sihusiki na
makosa. Nitaiacha Somalia ikiwa vizuri kuliko
nilivyoikuta," alisema.

Mchimba Riziki

Serikali Yatangaza Vita Ya Ukatili Wa Kijinsia na Watoto.

Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi
alitangaza mpango huo wakati wa Siku 16 za
kampeni ya Harakati Dhidi ya Unyanyasaji wa
Kijinsia, kampeni ya kimataifa inayolenga kuinua
uelewa kuhusu suala hili.

Takribani asilimia 45 ya wakina mama wenye
umri wa miaka kati ya miaka 15 hadi 49 waliripoti
kunyanyaswa kimwili au kijinsia katika maisha
yao, kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na
Afya nchini Tanzania wa mwaka 2010.

Watoto nao wako katika hatari kubwa, msichana
mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati
ya saba wamenyanyaswa kijinsia, na zaidi ya
asilimia 70 walinyanyaswa kijinsia kabla ya
kufikisha umri wa miaka 18.

"Jeshi la polisi linawajibika kuboresha mwitikio
wake kwa manusura wa [ukatili wa kijinsia] na
unyanyasaji wa watoto," Inspekta Jenerali wa
Polisi Said Mwema alisema.

Mchimba Riziki

NI LAZIMA UHURU AHUDHURIE KESI YAKE KAMA ILIVYOPANGWA NA ICC.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya
Jumanne (tarehe 26 Novemba) iliubadili uamuzi
ambao ungelimruhusu Rais Uhuru Kenyatta
kuhudhuria sehemu ya kesi yake, badala yake
ikasema kwamba Kenyatta "kwa ujumla lazima
awepo mahakamani", liliripoti shirika la habari la
AFP.

"Maombi yoyote hapo baadaye ya kuruhusiwa
kutohudhuria sehemu ya kesi yake yatazingatiwa
kwa msingi wa kesi na kesi," ilisema mahakama
hiyo ya ICC yenye makao yake mjini The Hague
katika taarifa yake.

Siku ya tarehe 18 Oktoba, majaji walimruhusu
kwa sehemu fulani Kenyatta kutohudhuria kesi
zake ili ashughulike na matokeo ya kuzingirwa
kwa jengo la maduka la Westgate jijini Nairobi
na al-Shabaab mwezi Septemba ambako kiasi
cha watu 67 walikufa.

Majaji wa ICC siku ya Jumanne waliamua
kwamba kutokuwepo kwa Kenyatta
"kutaruhusiwa tu katika mazingira maalum na
lazima kuwe kwa yale tu ambayo ni ya lazima."

Mchimba Riziki

Thursday, November 14, 2013

KAMA UNA MACHOZI YA KARIBU USISOME..!! SIMULIZI YA KWELI YA KUSISIMUA NA KUSIKITISHA YA MTOTO JANETH..!!

KAMA UNA MACHOZI YA KARIBU
USISOME..!! SIMULIZI YA KWELI
YA KUSISIMUA NA KUSIKITISHA
YA MTOTO JANETH..!!

Kengele ya kutoka darasani iligongwa,
wanafunzi wa shule ya msingi wakaanza
kutoka madarasani huku wakifukuzana
wengine wakipiga kelele ilimradi shwangwe
tu.

Ilikuwa mara yangu ya kwanza kufundisha
shule za hatua hiyo.
Ilikuwa ni shule ya serikali.
Jicho langu liliangukia katika sura ya
msichana mdogo, nguo zake chafu. Alikuwa
analia.
Alikuwa peke yake na hakuwa na yeyote wa
kumbembeleza.
Mimi kama mwalimu sikutaka kujisogeza
karibu naye sana. Kwanza nilikuwa mgeni.
Nikaachana naye.

Siku iliyofuata tukio kama lile likajirudia.
Msichana yuleyule wakati ule uleule wa
kutawanyika, alikuwa analia sana.
Mwishowe aliondoka huku akiwa analia.
“Mbona mwenzenu analia?” nilimuuliza
mwanafunzi mmoja.
“Huyo ni mama kulialia..” alinijibu huku
anacheka.

Haikuniingia akilini hata kidogo kuwa yule
binti analia bila sababu.
Siku ya tatu nikaanza kujiweka karibu naye.
Muda wa mapumziko nilimwita
nikamnunulia chai, alikuwa ananiogopa na
hakutaka kuniangalia machoni.
Sikumuuliza lolote juu ya tabia yake ya kulia
lia kila anaporuhusiwa kurejea nyumbani.

Hata siku hiyo pia alilia vilevile. Wenzake
wakawa wanamzomea.
Akili yangu iligoma kuamini kuwa binti yule
analia bila sababu.
Kwanini alie wakati wa kutawanyika tu??
Hapana si bure.
Nikaendelea kujiweka karibu naye. Mkuu wa
shule akafikishiwa taarifa kuwa nina
mahusiano ya kimapenzi na yule mtoto.

Moyo wangu na Mungu pekee ndio walikuwa
mashahidi. Nilikosa cha kujibu.
Nilijaribu kujiweka mbali naye lakini moyo
ulinambia kuwa kuna jambo natakiwa
kulijua.

Nikaendelea kuwa karibu naye. Hatimaye
mkuu wa shule akanisimamisha kufundisha
pale kwa tabia yangu ya kufanya mapenzi na
mwanafunzi.
Nilijitetea lakini sikueleweka. Nikamwachia
Mungu……
Licha ya kusimamishwa kazi, niliendelea
kufuatilia nyendo za yule binti aliyeitwa
Janeth.
Kila alipotoka shule nilimvizia njiani na
kumnunulia chakula, kisha tunazungumza
kidogo.

Aliponiamini kama kaka yake ndipo
nikajieleza dukuduku langu.
“Janeth…” nilimuita.
“Bee kaka ….” Aliitika huku akinitazama.
“Nyumbani unaishi na wazazi.”
“Ndio naishi na mama..baba huwa anasafiri
safari.”

“Mama yako ana watoto wangapi?”
“Mama yangu alikufa….alikufa nikiwa mdogo
hata simkumbuki” Alijibu kwa sauti ya chini.
“Kwa hiyo unaishi na mama mdogo.”
“Ndio.”
“Unampenda mama mdogo?”
Swali hili likaikatisha furaha ya Janeth.
Akaanza kulia, alilia bila kukoma, Janeth
alilia kwa uchungu hadi nikajisikia vibaya.
Nilimbembeleza kisha sikumuuliza tena.

Siku zikaenda bila kumuuliza chochote..
Baada ya siku kumi, ilikuwa siku ya michezo
pale shuleni, hivyo hapakuwa na masomo.
Janeth alichelewa kuja shule, nilimngoja
uwanjani, hadi alipofika majira ya saa nne.
Nikamwambia twende kunywa chai.
Siku hiyo nilimpeleka mbali kidogo,
tukanywa chai, kisha tukakaa mahali
palipokuwa wazi.
Nikaleta tena mjadala mezani.
Ni kuhusu maisha ya Janeth.
Alikataa kabisa kusema lolote, nilimshawishi
sana.

“Usiogope mimi ni kaka yako.” Nilimpooza.
Janeth badala ya kusimulia akaanza kulia
tena.
“Ataniua mama nikisemaaaa” alilalamika.
Nikambembeleza hatimaye akanieleza jinsi
anavyonyanyaswa na mama yake.

“Mama hanipendi hata kidogo, ananipiga na
kuninyima chakula, hapendi nije shule,
vyombo tunavyotumia usiku hataki nivioshe
usiku na hataki niwahi kuamka asubuhi,
nikiamka natakiwa kufanya kazi zote,
kufagia uwanja, kudeki nyumba, kuosha
vyombo kisha ndipo nije shule. Baba
akiwepo anajidai kunijali sana…”
Alijieleza.
“Ni hayo tu Janeth….niambie kila kitu.”
“Akijua ananiua alisema….”
“Kwani amewahi kukutesa vipi..”
Ni hapa Janeth alivyozungumza huku analia
kilio ambacho hakitatoka masikioni mwangu
kamwe.

Siku moja, alichelewa kuamka, ilikuwa siku
ya mapumziko.
Mama yake alipomwamsha, aliitika na
kupitiwa usingizi tena.
Mama aliporejea mara ya pili, alikuwa na mti
mkavu, alimpiga nao kichwani na popote
pale katika mwili, alipoona hiyo haitoshi
akamvua nguo, akausokomeza katika sehemu
za siri, aliuigiza hovyohovyo, ukuni huo
ulikuwa wa moto.

Yeyote mwenye moyo wa nyama ajifikirie
ukuni wa moto ukazamishwa sehemu za siri
za mtoto wa darasa la sita.
Nilitokwa machozi.
Nikawahi kujifuta hakuona.
“Baba yeye alisemaje….”
“Baba ni mkali na hapendi kunisikiliza na
mama aliniambia nikiambia mtu ananiua
mara moja.” Alijibu kwa huzuni.
“Nikija na dada yangu tunaweza kukuona
ulivyounguzwa..”
“Ndio…” alinijibu.
Sikutaka kulaza damu nikampigia simu rafiki
yangu wa kike.
Nikamuuliza kama yupo kwake, alikuwepo.

Nikaongozana na Janeth.
Tukafika, Janeth akatoa nguo zote.
Ilihitaji moyo wa kiuaji sana kutazama mwili
wa Janeth mara mbilimbili.
Alitisha, hakika alikuwa ameunguzwa vibaya
na vidonda vilikuwa havijapona vizuri.

Dada yule alishindwa kujizuia alimlazimisha
Janeth twende kwa mama yake amkabiri na
kumpa kipigo. Nikamzuia.
Hata mimi nilikuwa na hasira kali. Lakini
sikutaka kuiruhusu ifanye kazi.
Nikachukua kamera, nikampiga picha Janeth
katika yale makovu.

Mbio mbio nikaenda polisi, kituo cha haki za
watoto nikaelezea mkasa ule huku
nikishindwa kujizuia machozi.
Nikawaonyesha na picha.
Tukaongozana nao hadi nyumbani kwao
Janeth.
Mama yule akakamatwa bila kutarajia.
Nilitamani kumrukia nimng’ate lakini
haikuruhusiwa.
Sheria ikafuata mkondo. Janeth akaanza
kupokea tiba.

Yule mama akahukumiwa kwenda jela miaka
sita..hadi sasa yupo jela.
Mume wake alitozwa faini kubwa kwa kosa
la kutofuatilia maendeleo ya mtoto wake
kiafya……..

Mimi nilirudishwa kazini, kwa heshima
kubwa. Heshima ya nkumkomboa mtoto.

***Akina JANETH wapo mtaani
kwako…..usiwaangalie na kuwaacha tu…
hebu jaribu KUWA SAUTI YAO… .hawawezi
kusema…hebu sema badala yao…….wanalia
kisikie kilio chao…….

KAMA UMEGUSWA NA MKASA HUU SHARE
NA NDUGU JAMAA NA
MARAFIKI ZAKO ILI WAONE.

SOURCE Kandilihuru Blog.

Warioba Atoa Rambirambi kwa Familia Ya Dr Mvungi

Wakili wa Tanzania na mjumbe wa Tume ya
Kupitia Katiba (CRC) Sengondo Mvungi ,
aliyekuwa amejeruhiwa vibaya mapema mwezi
huu Alipovamiwa nyumbani kwake karibu
na jiji la  Dar es Salaam, alifariki siku ya Jumanne katika hospitali moja
nchini Afrika Kusini.

Kiasi cha watu sita wanaoshukiwa kuwa wezi
waliokuwa wamebeba mapanga walimshambulia
Mvungi nyumbani kwake siku ya tarehe 2
Novemba.

Alipelekewa kwa haraka kwenye
Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam ambako alikuwa kwenye
chumba cha wagonjwa mahututi hadi tarehe 7
Novemba,
aliposafirishwa kwenda Hospitali ya
Milpark jijini Johannesburg kwa matibabu zaidi.
Polisi hadi sasa wamewakamata washukiwa tisa.

Mwenyekiti wa CRC, Jaji Joseph Warioba,
alipeleka salamu zake za rambirambi kwa
familia ya Mvungi. "Alikuwa mtafiti ambaye
daima alikuwa na hamu ya kile alichokifanya.

Nilimjua na kufanya naye kazi hata kabla ya
kuwa mjumbe wa CRC, hivyo kifo cake kwa kweli
kimeniumiza," alisema Warioba.

Washukiwa Wawili Wa Ugaidi Wauwa Eastleigh Nairobi.

Polisi ya Kenya hapo jana walifanikiwa  kuwapiga risasi na kuwauwa watu
wawili wanaoshukiwa kuhusika na mashambulizi
dhidi ya msikiti mmoja uliopo Jam Street
Eastleigh, jijini Nairobi, mwaka jana,

"Ni vijana na tumepata guruneti la mkono na
bastola moja kutoka kwao. Tunaamini walikuwa
sehemu ya genge kubwa ambalo limekuwa
likiwatisha watu," alisema Kamanda wa Polisi wa
Kaunti ya Nairobi, Benson Kibui.

Washukiwa hao waliuawa karibu na kituo cha
kurekebisha magari yaani Garrage  hapa Eastleigh.

Bado haifahamiki kama
walikuwa wanadhamiria kutumia bomu hilo
kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Walikuwa wanasindikizwa na kijana wa tatu,
ambaye polisi sasa wanamtafuta, alisema Kibui,
kwa mujibu wa kituo cha Capital FM.

Wanaaminika kuwa sehemu ya kundi
linalohusika na mashambulizi dhidi ya waumini
waliokuwa wakitoka kwenye msikiti wa Al Hidaya
baada ya sala ya Ijumaa mwezi wa Disemba
2012, ambapo watu watano waliuawa na 16
kujeruhiwa, akiwemo mbunge wa Kamukunji,
Yussuf Hassan.

Mashambulizi dhidi ya raia hapa Eastleigh yalikithiri mwishoni  mwaka jana kwa kundi lisilojulikana kushambulia
Sehemu yenye mkusanyiko ya watu wengi lakini polisi wa kulinda raia walithibiti hali hiyo mpaka sasa hali ya usalama wa kutosha ipo katika mtaa huu.

Mchimba Riziki

Tuesday, November 12, 2013

Ligi Kuu Somalia Yashika Kazi.

Mchimba Riziki Michezo.

Ligi Kuu ya Somalia ilianza kwenye Uwanja wa
Michezo wa Benadir, Mogadishu, siku ya Ijumaa
(tarehe 8 Novemba), kwa mechi ya kwanza kati
ya timu za Heegan na Gaadiidka kumalizika kwa
ushindi wa 3-2 wa Heegan.

Ligi hiyo kuu inafanyika kwenye uwanja wa
kisasa ukiwa na nyasi bandia kwa mara ya
kwanza baada ya shirikisho la mpira la
kimataifa, FIFA, kuufanyia matengenezo Uwanja
wa Benadir .

Timu nane za mpira wa miguu za Somalia
kutoka mikoa ya Benadir, Shabelle ya Chini na
Shabelle ya Kati zitashiriki kwenye ligi hii, Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Somalia, Abdiqani Said Arab, alidokeza.

"Uwanja wa Michezo wa Benadir ulijengwa
mwaka 1956, lakini ukakumbwa na maharibiko
makubwa [wakati wa vita vya wenyewe kwa
wenyewe]," alisema Arab. "Hata hivyo, baada ya
matengenezo yaliyofanyika miaka miwili iliyopita,
umeboreshwa na kuwa na viwango vya kisasa.
Matengenezo hayo yalimalizika tarehe 1
Novemba, na ligi kuu ilianza tarehe 8
Novemba."

"Naishukuru FIFA kwa kuweka nyasi za bandia
uwanjani hapo, ambazo zinakidhi viwango vya
kimataifa kwa kipimo na ubora wake,"
aliongeza.
Alisema matengenezo hayo ya uwanja
yanazifanya mechi ziwe bora zaidi.

"Kutakuwa na ongezeko la vipaji vya
wanariadha, hamasa ya mashabiki na uzuri wa
uwanja. Sasa tuko kama yalivyo mataifa
mengine duniani na tuna fursa sawa kama
walizonazo," alisema.

Arab alisema sasa wako kwenye mchakato wa
kupanga matengenezo ya viwanja vingine kwani
uwanja mmoja hautoshi kwa mechi za mpira wa
miguu nchini Somalia.
"Matengenezo ya uwanja huu yalipokamilika,
tuliiomba FIFA kutengeneza uwanja mwengine,"
alisema. "Walikubali na tunataka kuufanyia
matengenezo uwanja wa [Chuo Kikuu cha Taifa
cha Somalia]," alisema, akiongeza kwamba
watajaribu kuhakikisha matengenezo
yanafanyika kwenye viwanja vingine hadi wawe
wametengeneza viwanja kumi.

Wasomali Nusu Millioni Kurudishwa Somalia

Wakimbizi wa Kisomali nchini Kenya
wanalazimika tu kurudi nyumbani kwa hiari,
ulisema Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu
(tarehe 11 Novemba) baada ya kusaini makubali
yanayolainisha hofu ya kuwepo urudishwaji wa
lazima wa wakimbizi zaidi ya nusu milioni .

"Urejeshwaji wa wakimbizi lazima ufanyike kwa
usalama na heshima," alisema Raouf Mazou,
mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa
Mataifa (UNHCR) nchini Kenya, akiongeza
kwamba shirika hilo litasaidia katika kuandaa
uhamishwaji huo ikiwa tu "hali iko sahihi,"
liliripoti shirika la habari la AFP.
Makubaliano hayo ya pamoja - yaliyowekwa
saini siku ya Jumapili jijini Nairobi na Kenya,
Somalia na UNHCR - yanakuja kukiwa na hofu
za mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya
wakimbizi wa Kisomali kufuatia al-Shabaab
kulizingira jengo la maduka la Westgate mnamo
mwezi Septemba .
Tume yenye wawakilishi kutoka pande zote tatu
itaamua lini uhamishwaji huo uanze na kiasi gani
cha pesa anakachohitaji kila mkimbizi
atakayehamishwa ili kufanikisha kipindi cha
mpito.
"Serikali ya Somalia itaendelea kujenga
mazingira salama kwa wakimbizi kurudi nchini
Somalia ili kuwawezesha kujiimarisha kwa
wepesi na kujenga upya maisha yao, wakiwemo
wakimbizi milioni 1.8 wa ndani ya Somalia,"
alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia,
Fowsiyo Yusuf Haji Aadan, wakati wa kuwekwa
saini kwa makubaliano hayo, kwa mujibu wa
gazeti la The Standard la Kenya.

By Mchimba Riziki

Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Kenya Aitembelea Tanzania Kuitoa Shaka Juu Ya Suala La Kutengwa EAC

Dar es salaam, Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina
Mohamed, ametetea mkutano wa Kenya na
Rwanda na Uganda mjini Kigali mwezi uliopita
bila ya wanachama wenzao wa Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki (EAC) Burundi na Tanzania ,
liliripoti gazeti la Daily News la Tanzania siku ya
Jumatatu (tarehe 11 Novemba).

Mohamed, aliyekwenda jijini Dar es Salaam siku
ya Jumapili, alisema mkutano huo ulijadili
masuala yenye maslahi ya moja kwa moja ya
pande hizo mbili na kulenga kwenye maeneo
ambayo yanaweza kuwa yaliachwa kwenye
mkutano wa kikanda wa EAC.

Mkutano huo ulijadili ukosefu wa ufanisi wa
bandari ya Mombasa ambao ulikuwa ukiziathiri
Rwanda na Uganda ambazo hazina bahari,
alisema Mohamed, akiongeza kwamba ulifanyika
kwa mujibu wa sheria za jumuiya ya EAC na
hauakisi kutengwa kokote kwa wanachama
wengine.

Pia aliisifu hotuba ya hivi karibuni ya Rais Jakaya
Kikwete wa Tanzania ambayo ilizikosoa Kenya,
Rwanda na Uganda kwa "kujibagua zenyewe "
kutoka wanachama wengine wa EAC kwa
kuunda "muungano wa wenye dhamira" na
kusaini makubaliano kati yao.

Alisema Kenya itahakikisha inaimarisha
mafungamano na wanachama wote wa EAC
katika siku zijazo. "Tutafanya kila tuwezalo
kuhakikisha kwamba EAC inaimarika chini ya
mataifa matano wanachama wa EAC na kuleta
maendeleo kwa watu wote," alisema Mohamed.

By Mchimba Riziki

Vyombo Mbalimbali Vyazidi Kuipinga Mswada Wa Sheria Kwa Vyombo Vya Habari Kenya, Uhuru Akataa Kuitia Saini.

Nairobi, Kenya

Sauti za kutoelewana zinaendelea kuongezeka
juu ya mswada wenye utata wa vyombo vya
habari ambao bunge la Kenya liliupitisha
mwishoni mwa mwezi uliopita, huku ikiripotiwa
kwamba rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
aliurudisha kwenye chombo cha kutunga sheria
kufanya mabadiliko.

Mswada wa Habari na Mawasiliano wa Kenya
(marekebisho) wa mwaka wa 2013, ambao
unahitaji saini ya Kenyatta kuwa sheria,
umeweka faini kubwa ya hadi shilingi milioni 1
(dola11,700) kwa mwandishi wa habari binafsi
na shilingi milioni 20 (dola 234,000) kwa chombo
cha habari kwa ukiukaji wa kanuni za maadili.
Waandishi wa habari pia wangepewa adhabu
kwa kufutiwa usajili na akaunti zao za benki
kufungwa.

Watunga sheria ambao walipitisha sheria hiyo
pia waliunda Mahakama ya Rufaa ya
Mawasiliano na Vyombo vya habari, iliyopewa
jukumu la kusikiliza malalamiko na kutoa
adhabu kwa waandishi wa habari
watakaogunduliwa kuvunja sheria.
Hivi sasa
Baraza la Vyombo vya habari la Kenya
hushughulikia malalamiko kama hayo.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
iliteua wajumbe wa mahakama hiyo, ambayo
kazi yake ni kuunda kanuni za maadili kwa
waandishi wa habari na vyombo vya habari.

"Kwetu sisi, hii ni sheria ya uonevu ambayo
inarudisha nchi nyuma kwenye enzi za giza,"
alisema Sekou Owino, mkuu wa huduma za
kisheria wa kampuni ya Nation Media Group.
Ukweli kwamba mahakama imeundwa na
wateuliwa wa serikali, pasipo wawakilishi wa
waandishi wa habari, inalifanya lisiwe huru
hususani wakati serikali inapokuwa na maslahi
na suala hilo, aliteta.
:
Mswada huo pia unahitaji vyombo vya habari
kutumia asilimia 60 ya programu zake kwenye
"habari za ndani ya nchi", alisema. Hili ni suala
lenye ubishi kwa sababu mswada huo
haufafanui "habari za ndani ya nchi" na mahitaji
hayo yanaingilia uhuru wa vyombo vya habari,
aliongezea.
Kenyatta na Ruto wajibu kuhusiana na
wasiwasi
Wakati alipojitokeza katika Kaunti ya Kajiado
tarehe 2 Novemba, Kenyatta alisema hatasaini
mswada wa sheria hadi masuala yenye ubishi
yashughulikiwe.
"Tunakusudia kushawishi vyombo vya habari
kama hiki kuwa mstari wa mbele katika uhuru
wa kujieleza ambao wote tunaupigania," alisema
Kenyatta.

Siku ya Ijumaa (tarehe 8 Novemba), Makamu wa
Rais William Ruto alikariri kusudio la rais.
"Bunge letu lilipitisha mswada ambao tunakubali
una ubishi," aliliambia kusanyiko la viongozi wa
vyombo vya habari Afrika katika mji mkuu wa
Ethiopia Addis Ababa, kwa mujibu wa AFP.

"Rais wa Kenya amerejesha mswada kwa bunge
ili masuala haya yashughulikiwe," alisema,
akiongeza kwamba "mjadala unaandaliwa kati
ya wadau mbalimbali -- bunge la utendaji na
vyombo vya habari -- kutatua masuala yenye
ubishi."

"Uhusiano kati ya serikali na vyombo vya habari
hauhitaji ushindani," alisema Ruto.
Sheria ina lengo la 'kuwanyamazisha
waandishi wa habari'
Lakini wawakilishi wa vyombo vya habari na
wawakilishi na watetezi wanaendelea kuukosoa
mswada huo.

Kifungu cha 19, shirika la utetetezi wa haki za
binadamu lenye makao makuu huko London
ambalo linapambana na udhibiti wa habari na
kukuza uhuru wa kujieleza na wa habari.
aliielezea sheria hiyo kuwa ni ya "kizamani".
Muswada huo unakiuka vifungu vya katiba ya
Kenya na kuanzisha vifungu vya viwango vya
kimataifa vya habari, Mkurugenzi wa Kifungu
cha 19 Pembe ya Africa Henry Maina alisema.

Katiba ya Kenya inahakikisha "uhuru na
kujitegemea kwa vyombo vya habari vya
kielektroniki, uchapishaji na aina nyengine za
habari".
"Taifa halitapaswa kutekeleza udhibiti au
kuingilia kati mtu yeyote anayajihusisha na
utangazaji, utoaji au usamabazaji wa chapisho
au usambazaji wa habari kwa njia yeyote; au
kuadhibu mtu yeyote kwa maoni au mtazamo
wa yaliyomo katika habari, chapisho au
usambazaji wa habari," inaeleza.
"Lakini kile ambacho bunge imepitisha ni jaribio
la makusudi la serikali na vyombo vyake
kudhibiti vyombo vya habari kinyume na katiba,"
Maina alisema.

"Kuna vitisho vya kutosha kwa jina la usalama
wa taifa, ambapo katika hali halisi serikali
inataka kufunga nafasi za kidemokrasia za
watu," Mwenyekiti wa Chama cha Sheria cha
Kenya Eric Mutua alisema. "Hili
linapaswa kupingwa na Wakenya wote."

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wahariri wa
Kenya David Ohito alisema ukali wa adhabu kwa
uvunjaji wa sheria unaweza kusabibisha vituo
vya redio na kampuni nyengine za vyombo
vyengine kufungwa kwa sababu vingi vyao
haviwezi kulipa faini hizo zinazotarajiwa.

"Kile ambacho sheria imetolewa ni
kuwanyamazisha waandishi wa habari na
vyombo vya habari, kumaanisha kwamba
wananchi hawatakuwa na uwanja wa kujielezea
kwa uhuru dhidi ya watawala wasiokuwa
wawajibikaji. Inamaanisha kwamba nchi nzima
itakuwa imenyimwa haki ya kuieleza uhuru,"
Ohito alisema.

"Nyingi ya kampuni zetu za habari zina bajeti ya
uendeshaji kwa mwaka chini ya shilingi milioni
40 [dola 468,000]," alisema. "Ikiwa utavitwanga
na angalau faini tatu kila mwaka, maana yake
utakuwa umekula bajeti yao yote. Hawatakuwa
na chaguo lingine zaidi ya kufunga."

Na, adhabu ambazo waandishi wa habari binafsi
wanazoweza kukabiliana nazo, pia zitakuwa
kubwa mno, alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maripota wa Kenya, William Oloo Janak.
"Faini hizi ni kubwa kupita kiasi," Janak alisema . "Hakuna sheria nyengine yeyote katika
nchi hii ambayo ina faini kubwa ya utovu wa
adabu kibinadamu inayoamuliwa na mahakama.
Kwa sisi, hili ni jaribio la serikali la
kuwanyanyasa waandishi wa habari."

'Hakuna chochote cha kibabe au kinyume
na katiba katika mswada'
Hata hivyo, Jamleck Kamau, mbunge ambaye
aliupeleka mswada huo katika Bunge la Taifa,
alivishutumu vyombo vya habari vya Kenya kwa
kupotosha ukweli.

"Suala hili limekuwa likitangazwa vibaya. Kwa sisi
hakuna chochote cha kibabe au kinyume na
katiba katika mswada huo," Kamau, ambaye pia
ni mwenyekiti wa kamati ya Mawasiliano na
Habari ya bunge alisema.

"Tunawaomba rais kutia saini iwe sheria kama
ilivyo kwa sababu vipengele vya vilivyomo humo
ni vizuri kwa nchi hii kwa kuwa vitavifanya
vyombo vyetu vya habari kuwajibika zaidi na
kuwa na malengo katika kazi yao ambazo kwa
upande mwengine utaibadilisha Kenya," alisema.
"Inapotosha kweli [kusema] kwamba Mahakama
ya Rufaa ya Mawasiliano na Vyombo vya habari
itakuwa na nguvu kupita kiasi za kuwatia
mbaroni waandishi wa habari na kuvamia ofisi
za vyombo vya habari. Lakini kama tulivyosema
kabla, suala hili limetatuliwa na mswada umo
njiani kuelekea kuwa sheria," alisema, na
kukataa kufafanua zaidi.

Mchimba Riziki

Tuesday, November 5, 2013

Wabunge wa Tanzania wapinga kanuni mpya ya maadili ya kazi

Wabunge wa Tanzania wametoa kauli ya kupinga
kanuni mpya ya maadili ya kazi iliyotolewa na
afisi ya Spika wa Bunge, kwa kusema kwamba
inakandamiza nguvu za kikatiba za wabunge za
kusimamia na kuishauri serikali.
Ofisi ya Spika wa Bunge ilisambaza kanuni hiyo
mpya siku ya Ijumaa (tarehe 1 Novemba).

Inakusudia kuzuia vurugu ndani na nje ya
bunge, kufuatilia tabia za wabunge na kuwazuia
wabunge kupokea au kutoa rushwa.
Wabunge wanaunga mkono kanuni hiyo kwa
jumla, lakini wanapingana na kutakiwa kuomba
ruhusa kutoka kwa maafisa wa serikali ili kuweza
kuona nyaraka za siri, jambo ambalo huko
nyuma haikuwa hivyo.

Deo Filikunjombe, mbunge kutoka chama tawala
Chama Cha Mapinduzi, alisema kuwa dhamiri ya
kanuni mpya ya maadili ya kazi ilikuwa nzuri,
lakini inavuka uwezo wake wa kisheria kwa
kujaribu kukiuka katiba ya nchi.
"Kifungu cha 63 (2) cha katiba yetu kiko wazi
kabisa. Kinasema kwamba mbunge atakuwa na
mamlaka kwa niaba ya watu, kusimamia na
kuishauri serikali ya jamhuri ya muungano,"
Filikunjombe alisema siku ya Jumatatu.
"Sasa, inakuwaje yule unayemtarajia
kumsimamia anatoa masharti ya kukupa habari
kwa kujisikia kwake?"

Godbless Lema, mbunge kutoka chama cha
upinzani Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
alisema kwamba kanuni hii imeundwa
ili kuwanyamazisha wabunge wa upinzani
ambao wamekuwa wana uwezo wa kuangalia na
kutumia nyaraka za siri ili kuilazimisha serikali
iwajibike.

"Watakuwa wanajidanganya wao wenyewe
kufikiria kwamba wanaweza kutuzuia kirahisi
sana," Lema alsema. "Ikiwa itapitishwa kwa
sababu chama tawala kina wingi wa kura
bungeni, sisi tutawaambia wapiga kura kwamba
serikali imejigeuza kuwa ufalme na nina hakika
kwamba haitachaguliwa tena.

Tunataka serikali
yenye uwazi."
Kanuni mpya ya maadili ya kazi imepangwa
kujadiliwa bungeni wiki hii.

Thursday, October 31, 2013

Kitengo cha kupambana na ujangili Tanzania chatuhumiwa kwa kukiuka haki za binadamu

Kampeni ya kupambana na ujangili Tanzania
imeingia matatani baada ya tuhuma za ukiukaji
wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na
kuteka nyara na kuua mwanamke, gazeti la The
Citizen la Tanzania liliarifu hapo Jumatano
(tarehe 30 Oktoba).

Kitengo cha kupambana na ujangili,
kinachojumuisha polisi, jeshi na maafisa wa
kiintelijensia, kilidaiwa kumtia kizuizini Emaliana
Gasper Maro, mwenye umri wa miaka 46, siku
kadhaa baada ya kumkamata mume wake Elias
Kibuga, mwenye umri wa miaka 56. Kibuga
amekuwa haonekani tangu alipochukuliwa kwa
ajili ya kuhojiwa, lakini mwili wa Muro
ulionekana katika mochuari ya Hospitali ya
Mirara.
Watu wengine wengi wanaripotiwa kutoonekana,
na maafisa pia wanashukiwa kwa kuwachomea
moto nyumba zao.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara Akili
Mpwapwa alithibitisha ripoti hizo na kusema
uchunguzi ulikuwa unaendelea.
Joseph ole Parsambei wa Jukwaa la Wachungaji
Tanzania alisema kwamba kitengo cha
kupambana na ujangili pia kilikuwa
kinawashikilia wachungaji 27 na mifugo 2,169.
"Tutakwenda mahakamani kuzuia zoezi hili ikiwa
ukiukwaji wa haki za binadamu utaendelea,"
alisema.
Waziri wa Maliasili na Utalii Khamis Kagasheki,
ambaye aliripotiwa kuanzisha kampeni ya
kupambana na ujangili, alikataa kutoa maoni
yoyote.

12 wafa wakati basi ilipogongana na treni Nairobi

Watu 12 walikufa na wengine kadhaa kujeruhiwa
baada ya treni ya abiria kuligonga basi kwenye
makutano ya reli jijini Nairobi siku ya Jumatano
(tarehe 30 Oktoba), walisema maafisa wa polisi.

Ajali hiyo ilitokea kwenye wilaya ya Eastlands,
Nairobi, wakati barabara zikiwa zimejaa watu
katika kipindi cha pilika pilika  nyingi za magari
asubuhi, alisema kamanda wa polisi wa eneo
hilo, Benjamin Nyamae, kwa mujibu wa shirika
la habari la AFP.
"Basi hilo lilipita mstari wakati treni likija kwa
kasi kubwa," alisema Mkuu wa Polisi wa Nairobi,
Benson Kibui.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema
abiria 34 walijeruhiwa na kupelekwa kwenye
Hospitali ya Mama Lucy kwa ajili ya matibabu na
17 wako kwenye Hospitali ya Taifa ya Kenyatta
kwa ajili ya matibabu maalum. Wengine wawili
wanatibiwa kwenye Hospitali ya MP Shah, kwa
mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.
"Tutafanya uchunguzi wetu kamili kwa
kushirikiana na polisi ili kujua kipi hasa
kimetokea," alisema mkuu wa kampuni ya Rift
Valley Railways, Darlan David. "Hata hivyo,
popote palipo na alama ya kukata njia, kanuni ni
kwamba magari yote husimama kupisha treni
inayokaribia kufika."
Dereva wa basi hilo, Edward Githae Wanjau,
mwenye umri wa miaka 43, yuko mikononi mwa
polisi na "atafikishwa mahakamani na
kushitakiwa kwa kusababisha vifo vya watu 12
na kujeruhi wengine kadhaa kwa kuendesha gari
katika hali ya hatari," alisema Mkuu wa Polisi,
David Kimaiyo, kupitia mtandao wa Twitter.

Wednesday, October 30, 2013

Maofisa wa Somalia wasifu shambulio la Marekani dhidi ya mtengenezaji bomu wa ngazi ya juu wa al- Shabaab

Msemaji wa waziri mkuu wa Somalia Ridwan
Haji Abdiwali alisema serikali ya Somalia ilikuwa
na taarifa kuhusu mipango ya Marekani
kumshambulia mtendaji mwandamizi wa al-
Shabaab Ibrahim Ali Abdi, ambaye pia
alijulikana kama Anta Anta, katika kijiji cha
Dhaytubaako.
"Tulifanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya
Marekani kufanya aina hizi za mashambulio,
kama tunavyofanya na yeyote yule [anayejaribu]
kuondoa kikundi hiki cha ugaidi,"
Anta Anta alihusika na misheni za kujitoa
mhanga za al-Shabaab na kuwa tishio kwa
umma, alisema Abdiwali, akiongezea kwamba
operesheni hiyo ilikuwa ni mafanikio kwa serikali
ya Somalia na watu wake.
"Tuna furaha [kuhusu matokeo ya shambulio
hilo] na tunayakaribisha," alisema. "Tuna
matumaini ya kuwazuia [watendaji] wengine
kama huyo."
Anta Anta anasemekana kujulikana vizuri kwa
kutengeneza fulana za milipuko na kutayarisha
mabomu ya kwenye magari yanayotumiwa mara
kwa mara na al-Shabaab.
Wakaazi waliokuwa karibu na eneo la
mashambulio waliripoti kuwa watu wapatao
watatu walikuwa kwenye magari yaliyoungua,
ambayo yalilipuka kwa moto muda mfupi baada
ya sauti ya ndege kusikika hewani, kwa mujibu
wa AFP.
Mashambulio ya ndege isiyo na rubani yalifuatia
operesheni nyingine ya Marekani ya mapema
mwezi huu, wakati kitengo cha wataalamu cha
makamanda wa Marekani kilipokuja kwenye
ufukwe wa mji wa Somalia ya kusini wa Barawe
katika jaribio la kumkamata Abdulkadir
Mohamed Abdulkadir "Ikrima" , Mkenya mwenye
asili ya Somalia na anayedaiwa kuwa kamanda
wa al-Shabaab wa wapiganaji wa nje.
Operesheni zote za Marekani zimekuja baada ya
uzingiraji wa siku nne wa al-Shabaab wa kituo
cha maduka ya biashara cha Westgate cha
Nairobi mwezi Septemba ambapo watu wapatao
67 waliuawa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia
Abdikarin Hussein Guled aliiambia Redio
Mogadishu kwamba shirika la upelelezi la nchi
yake limekuwa likimfuatilia Anta Anta kwa muda
fulani.
"Operesheni ambayo mtu huyu aliuawa ilikuwa
muhimu sana kwa serikali," alisema Guled. "Mtu
huyu alikuwa na dhima kubwa katika vifo vya
raia wengi wasiokuwa na hatia na kifo chake
kitasaidia kurejesha amani."
Kushirikiana na wabia wa kimataifa
Mbunge wa zamani Mohamud Weheliye Waqaa,
ambaye alitumikia katika Serikali ya Mpito ya
Shirikisho, alisema mashambulizi ya ndege
zisizokuwa na rubani ni njia nzuri ya
kuunganisha mafanikio ya usalama wa Somalia
na kuiunga mkono serikali ya Somalia.
"Serikali ya Somalia inapaswa kushirikiana
taarifa na [wabia] wanaofanya mashambulizi
hayo ili kuwatoa magaidi,"
Kwa kuzingatia ukweli kwamba jeshi la Somalia
bado halijafanikisha uwezo wa kiufundi kufanya
operesheni hizo, alisema, ni muhimu kwamba
jeshi la Somalia lifanye kazi kwa kushirikiana na
wabia wa kimataifa wakikusanya taarifa katika
maeneo huku wakiomba msaada wa kufanya
aina hizi za mashambulizi inapohitajika.
Hata hivyo, mbunge Mohamed Abdi Yusuf
alisema utawala wa Rais Hassan Sheikh
Mohamud haukupaswa kuidhinisha
mashambulizi hayo bila kushauriana kwanza na
bunge.
"Ubia kama huu unaohusisha ushirikiano kati ya
utawala na nchi za kigeni unapaswa
kuwasilishwa [kwa ajili ya mjadala] bungeni,"
Alisema mapambano yanaweza kusababisha
madhara ambayo hayakukusudiwa kama vile
vifo vya raia, hivyo makubaliano ya wazi
yanapaswa kufikiwa kabla ya kuanza.
Kuimarisha uwezo wa kiintelijensia
Wananchi wa Somalia pia wana maoni
mbalimbali kuhusiana na operesheni hiyo.
Sado Dahir, mwenye umri wa miaka 26
mwanafunzi wa sayansi ya jamii katika Chuo
Kikuu cha Somalia, alisema mashambulizi ya
kutumia ndege zisizokuwa na rubani yalikuwa
ushindi kwa umma wa Somalia.
"Kwanza, hii ni mara ya kwanza kabisa kumsikia
mtu mwenye jina hili, na mwanzo nilidhani
kwamba hakuwa maarufu sana ndani ya al-
Shabaab. Hata hivyo, niliposikia kwamba
alihusika katika kufanya milipuko, nilitambua
jinsi alivyokuwa hatari katika umma," "Hii ni operesheni nzuri sana ambayo
ilifanyika kwa mafanikio na ninaipongeza."
Dahir pia alisema ilikuwa ni muhimu kwa serikali
ya Somalia kuimarisha uwezo wake wa
kiintelijensia.
"Uimarishaji pekee hautafanikisha jambo lolote.
Kila shambulio lililofanyika dhidi ya al-Shabaab
linapaswa kuwa lililopangwa kwa makini ili
lifanikiwe kama hili, na serikali inapaswa
kufanya kazi na serikali zote duniani kuhusu
kuimarisha kitengo chake cha intelijensia,"
alisema.
Lakini Mohamed Jimale, mwenye umri wa miaka
57, alisema ingekuwa afadhali
kumkamata Anta Anta badala ya kumuua.
"Kama serikali ya Somalia na Marekani ilijua
kuhusu anakopatikana mtu huyu anayeitwa Anta
Anta ambaye ni mwanachama wa al-Shabaab,
ninadhani ingekuwa vizuri zaidi kumkamata ili
aweze kuhojiwa na kupata taarifa zaidi, kwani
yeye siye kiongozi hatari peke yake wa al-
Shabaab," alisema. "Hata hivyo, ninaunga
mkono jitihada za kupambana na kila kitu
ambacho kinaleta tishio katika umma."

By Mchimba Riziki

Friday, October 25, 2013

Kimaiyo Atishia Kuwakamata Waandishi Wa Habari Wakiwemo Wa KTN Ya Kenya

The truth Behind Westgate Siege

Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, amewatishia waandishi wa habari kwamba atawakamata baada ya kuripoti wizi na mkanganyiko miongoni mwa vikosi vya usalama wakati wa mzingiro wa al-Shabaab kwenye jengo la maduka la Westgate mwezi uliopita.

"Ni wazi kwamba kuna kikomo" cha uhuru wa kujieleza na haki za vyombo vya habari, Kimaiyo aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatano (tarehe 23 Oktoba).

"Hamuhitajiki kusambaza propaganda ya kivita, hamupaswi kuwachochea Wakenya, hamupaswi kusambaza au pengine kutoa taarifa ambazo zinaweza kuwa sawa sawa na kauli za chuki, na hamupaswi kutoa taarifa au ripoti ambazo zinaweza kuyaathiri maisha ya mtu mwengine," alisema.

"Tunawafuatilia kisheria kwa karibu sana wale watu ambao kwa njia moja ama nyingine wanaweza kuwa wametenda matendo ya kihalifu....ambao karibuni watatiwa nguvuni na kupelekwa mahakamani, na kukabiliana na matokeo ya jambo hili," alisema Kimaiyo.

Picha za kamera za usalama kutoka siku ya pili ya kuzingirwa kwa jengo hilo, ambapo ni jeshi tu lililokuwa na fursa ya kuingia kwenye jengo hilo, zinawaonesha wanajeshi wenye silaha wakibeba mifuko meupe ya plastiki kupeleka nje ya duka.

Licha ya hayo, Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya, Julius Karangi, alisema siku ya Jumanne kwamba wanajeshi hao walichukuwa vinywaji tu kwa ajili ya "kusinza kiu zao" na bidhaa nyingine "ili kuhakikisha usalama wake".

Waandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha KTN nchini Kenya ni miongoni mwa wale wanaoitishiwa kukamatwa.

Vyanzo vya polisi siku ya Alhamisi vilisema timu maalum imepewa jukumu la kuwahoji waandishi wawili wa KTN akiwemo Mohammed Ali. KTN ilisema kipindi chake maalum cha saa moja kinachochunguza mashambulizi ya Westgate kilimuudhi Kimaiyo.

Onyo hilo linakuja huku bunge likitayarisha mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari ambayo itawabana sana waandishi wa habari.

Chama cha Sheria cha Kenya kilisema sheria hiyo lilikuwa "jaribio la kuingilia haki ya kikatiba ya uhuru ya vyombo vya habari na kujieleza," huku Tume ya Haki za Binadamu ya nchi hiyo ikisema ilikuwa na "wasiwasi sana".

"Vyombo vya habari vinavyoinuka kwa kasi nchini Kenya havipaswi kuandamwa kwa sababu tu ya kutangaza ukweli," alisema Tom Rhodes wa Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari. "Badala yake, polisi wa Kenya wanapaswa kuchunguza wahalifu hasa wa Westgate, na sio wajumbe."

By Mchimba Riziki

Saturday, October 19, 2013

Uharamia Bado Ni Tishio Pembe Ya Afrika


Mashambulizi mawili ya kiharamia wiki iliyopita kwenye upwa ya Somalia yamezusha wasiwasi kwamba kitisho cha uharamia kwenye Pembe ya Afrika hakijaisha, liliripoti jarida la Seatrade Global siku ya Jumatano (tarehe 16 Oktoba).

Ijumaa iliyopita, maharamia waliokuwa kwenye mashua mbili waliirushia risasi meli ya mafuta inayopepea bendera ya Hong Kong, MV Splendor, likiwa ni tukio la kwanza la aina hiyo tangu mwezi Aprili, kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi wa Baharini la Dryad lenye makao yake nchini Uingereza. Siku nne baadaye, genge hilo hilo la maharamia liliishambulia meli nyengine kubwa umbali wa maili 270 za majini kutoka mahala yalipotokea mashambulizi ya awali.

"... Mashambulizi hayo dhidi ya meli mbili ndani ya kipindi cha siku nne yanathibitisha kwamba biashara ya uharamia ya Somalia bado haijavunjwa," alisema Ian Millen, mkurugenzi wa upelelezi wa Dryad.

Millen alisifu hadhari na utaalamu wa timu ya walinzi wa MV Splendor katika kukabiliana na mashambulizi hayo, ambapo walifanikiwa kukinusuru chombo, na kuzitolea wito meli nyengine kwenye eneo hilo kudumisha viwango vya hali ya juu vya ulinzi.

Hata hivyo, uharamia kwenye bahari uko kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miaka saba, liliripoti Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Baharini (IMB) siku ya Alhamisi. Kwenye upwa wa Somalia, kulifanyika mashambulizi 10 ya kiharamia katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu, ikilinganishwa na mashambulizi 70 kwenye kipindi kama hiki mwaka 2012, ilisema IMB.

"Jukumu kubwa linalotekelezwa na wanajeshi wa majini kwenye upwa wa Somalia halipaswi kudharauliwa. Kuwepo kwao kunahakikisha kwamba maharamia hawafanyi kazi zao wakiwa na hisia za kutokuchukuliwa hatua kama mwanzoni," alisema Mkurugenzi wa IMB, Pottengal Mukundan.

"Ingawa idadi ya mashambulizi imeshuka kwa ujumla, kitisho cha mashambulizi kingalipo, hasa kwenye bahari ya Somalia na Ghuba ya Guinea," alisema. "Ni muhimu kwamba manahodha wa meli waendelee kuwa na hadhari wanapopita kwenye bahari hizi."

By Mchimba Riziki

Uganda Yatishiwa Nayo Kushambuliwa Na Magaidi Waliishambulia Kenya

Kampala,Uganda
Magaidi walioishambulia Kenya na Kutishia kuivamia Tanzania na Rwanda sasa waigeukia Uganda ,hapo jana walitoa vitisho balaa kuhusina na suala la kutaka kuivamia Uganda saa yoyote ile. Jeshi la Uganda nalo lipo Rada kuwathibiti wasifanikiwe kufanya shambulizi lolote na kuleta hasara

Uganda ilikuwa kwenye hali ya tahadhari siku ya Ijumaa (tarehe 18 Oktoba) kutokana na hofu za mashambulizi kama yale ya al-Shabaab katika jengo la Westgate jijini Nairobi, ambako bado wapelelezi wanaendelea kufukua miili iliyooza takriban mwezi mzima baadaye, liliripoti shirika la habari la AFP.

"Kuweni na tahadhari na chunguzaneni hatua na matendo ya kila mmoja, kwani bado tunatishwa na ugaidi," ulisema ujumbe wa polisi ya Uganda, huku vikosi vya usalama vikifanya doria nje ya maduka kwenye mji mkuu, Kampala.

Hatua hii ilifuatia ujumbe wa siku ya Jumanne kutoka ubalozi wa Marekani nchini Uganda ambao ulisema ubalozi huo ulikuwa ukiendelea "kutathmini ripoti kwamba mashambulizi kama yale ya Westgate yatatokea mjini Kampala hivi karibuni". Ubalozi huo ulisema hakukuwa na taarifa zaidi juu ya wakati na mahala wa mashambulizi yoyote.

Siku ya Alhamisi, wapelelezi walipata fuvu la kichwa lililoharibika kwenye mabaki ya jengo la Westgate, walisema polisi wa Kenya, wakiongeza kwamba kipimo cha DNA kitafanywa ili kusaidia kulitambua. Bunduki pia zilipatikana.

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu 23 walipotea baada ya kuzingirwa kwa jengo hilo.

Kuna wasiwasi mkubwa kwamba al-Shabaab watatekeleza kitisho chao cha kufanya mashambulizi zaidi, baada ya wanamgambo hao wenye mafungamano na al-Qaida kusema kupitia mabango kwenye maandamano nchini Somalia kwamba "Westgate ulikuwa ni mwanzo tu."

Mkanda wa vidio ya propaganda pia ulitolewa wiki hii na al-Shabaab ukikipongeza kikosi chake cha wapiganaji wa kigeni, ukionesha waasi kadhaa ambao wanadaiwa kuwa walitoka Uingereza na waliouawa kwenye mapigano.

Hapana shaka, vidio hiyo ilifanywa kabla ya mashambulizi ya Westgate kwani haizungumzii mashambulizi hayo, ingawa inataja juu ya "mateso ya Waislamu nchini Kenya" na pia kwenye nchi nyengine.

Vidio hiyo inayosimuliwa na mwanamme aliyevalia sare ya kijeshi na uso wake ukiwa umezibwa kwa kitambaa na anayezungumza lafudhi ya Kiingereza safi, inadai wapiganaji kutoka mataifa kadhaa ikiwemo Ethiopia, Eritrea, Lebanon, India na Pakistan wote wamepigana upande wa al-Shabaab.

By Mchimba Riziki

Friday, October 11, 2013

Westgate Kukarabatiwa Kwa Upya

Serikali ya Kenya imetangaza mipango ya ujenzi wa haraka wa jengo la Westgate la Nairobi baada ya sehemu ya jengo hilo kuharibiwa kwenye mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na wanamgambo wa al-Shabaab mwezi uliopita.

Katika mkutano wake na wamiliki wa maduka jioni ya siku ya Jumatano (tarehe 9 Oktoba), Waziri wa Biashara wa Kenya, Phyllis Kandle, alisema anataka kuona kwamba Westage inarudi kwenye shughuli zake na akaahidi msaada wa serikali.

"Serikali ya Kenya imedhamiria kwa dhati kabisa kuhakikisha kwamba shughuli za jengo la Westgate zinarudi ndani ya kipindi kifupi kabisa kadiri inavyowezekana kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na ya binafsi," alisema.

"Kupitia ubia huu, tutakuwa tunajaribu kuhakikisha uwezo wa pamoja wa kuhimili kwenye uchumi ngazi ya taifa kufuatia matukio ya kusikitisha kwa kupunguza kiwango cha kuporomoka kwa biashara, imani ya wawekezaji na kupotea kwa nafasi za kazi," alisema.


Kabla ya mashambulizi hayo, jengo la Westgate lilikuwa likizalisha zaidi ya shilingi bilioni 100 (dola billion 1.2) kwa mwaka na likiwa limetoa zaidi ya nafasi 2,000 za ajira. Ripoti zinasema kwamba jengo hilo limekatiwa bima ya shilingi bilioni 6.6 (dola milioni 77), na sera ya kufidiwa madhara ya mashambulizi ya kigaidi.

Hata hivyo, bado haijawa wazi ikiwa kuna utafiti wowote uliokwishafanyika wa jengo hilo kuona ikiwa kuna madhara zaidi ya kimuundo kwenye kituo hicho cha biashara kilichosababishwa na moto na kuporomoka kwa ghorofa ya nne iliyokuwa na eneo la kuegeshea magari.

Vyanzo vilivyo karibu na uchunguzi unaoendelea vinasema itachukuwa angalau kiasi cha mwezi mmoja kusafisha kifusi, liliripoti shirika la habari la AFP. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema bado watu 39 hawajapatikana, na kuna hofu kwamba miili zaidi inaweza kupatikana kwenye mabaki ya jengo hilo.

By Mchimba Riziki

Wednesday, September 25, 2013

Uchambuzi kuhusiana na shambulizi la kigaidi nchini Kenya Katika duka la kifahari WestgatE Nairobi


Uchambuzi kuhusiana na shambulizi la kigaidi nchini Kenya Katika duka la kifahari WestgatE Nairobi:



Tukio hilo la kigaidi lilianza mchana wa Jumamosi wakati kikundi cha watu wenye silaha, walioripotiwa wakiwa wa mataifa kadhaa, walipoingia katika jengo hilo, kuweka maguruneti na kufyatua bunduki za automatiki, huku wakiua ovyo raia wasio na hatia na kuwafanya  wanunuzi waliochanganyikiwa kutoroka.

Vikosi vya usalama vya Kenya tangu wakati huo vimewekwa katika hali ya mapambano na wanamgambo hao.

Jeshi la Kenya siku ya Jumatatu lilisema kwamba limeshaokoa sehemu kubwa ya jengo la maduka, huku afisa mmoja wa usalama alisema kwamba uvamizi wa mwisho ulikuwa uko njiani dhidi ya ya wanamgambo wa al-Shabaab, wanaoaminika kuwa wamejificha katika sehemu ya duka hilo lakini wanawatumia mateka kama ngao yao.

Zaid ya watu 1,000 walisalimishwa tangu operesheni hizo zilipoanza.

Makisio yanawaweka watu waliouawa wakati wa mzingiro huo wa siku tatu za umwagaji damu kuwa zaidi ya 60, pamoja na takriban watu 200 kulazwa hospitali kutokana na majeraha ya bunduki na majeraha mengine, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema kwamba dazeni kadhaa zaidi waliarifiwa kutoonekana.

Al-Shabaab, ambao wamedai kuhusika na shambulio hilo, walisema kwamba shambulio hilo lilikuwa ni kulipiza kisasi kwa uvamizi wa jeshi la Kenya huko Somalia, ambako majeshi ya Umoja wa Afrika yanapambana na wanamgambo.

"Ikiwa mnataka Kenya yenye amani, hiyo haitatokea wakati watoto wenu wakiwa ndani ya ardhi yetu," msemaji wa al-Shabaab Ali Mohamud Rage alisema katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa wanajihad.

Rage alionya kwamba mateka "wataathirika kwa mashambulizi yoyote yatakoelekezwa dhidi ya mujahidina".

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, hata hivyo, aliapa kuwa washambuliaji "wasingesalimika na matendo yao ya kuchukiza na ya kinyama".

Katika hotuba kwa taifa kupitia televisheni siku ya Jumamosi usiku, Kenyatta aliyeonekana kushtushwa, alisema, "Tutawasaka wakosaji popote watakapokimbilia. Tutawapata na tutawaadhibu kwa uhalifu huu wa kutisha."

Kenyatta alisema kuwa shambulio hilo la kigaidi lilikuwa na athari ya moja kwa moja familia yake. Siku ya Jumapili, rais alibainisha kuwa mpwa wake Mwangi Mbugua na mchumba wake Rosemary Wahito waliuawa katika shambulizi hilo.

"Ninahisi maumivu kwa kila maisha yaliyopotea na ninaungana nanyi katika huzuni na upotevu wa taifa," Kenyatta alisema, na kuwaelezea jamaa zake waliouwawa kama "vijana, wenye upendo na mimi binafsi niliwajua na kuwapenda".

"Ugaidi ni falsafa ya waoga," alisema.

Westgate, moja ya maduka ya kisasa nchini Kenya, ilifunguliwa miaka sita iliyopita na iko katika eneo la Westlands, takriban kilomita 5 kutoka katikati ya jiji. Kituo hicho cha maduka chenye ukubwa wa futi za mraba 350,000 kinatembelewa na Wakenya wakwasi, wataalamu kutoka nje na watalii huku Jumamosi ikiwa siku ya harakati zaidi.

Hasira miongoni mwa Wakenya; viongozi waomba watu kujizuia, kuwa na umoja

Shambulio hilo limechochea hasira zilizoenea miongoni mwa Wakenya huku wengi wao wakielezea ka uwazi chuki zao dhidi ya Waislamu na raia wenye asili ya Somalia.

Viongozi wa kidini na wanasiasa, hata hivyo, wanaomba uvumilivu, umoja na kujizuia kulaumu sehemu zote za jamii.

"Ninaungana na familia za waliofariki na ninawatakia majeruhi wapone haraka," alisema Sharrif Mohamed Khatamy, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu la Kenya.

"Pamoja na hayo, ninawaomba Wakenya kuonesha uvumilivu na kuungana licha ya tofauti zao za kidini," alisema Sharrif. "Kilichotokea Westgate hakikubaliki. Ni matendo ya kudharaulika na ninayalaani kwa maneno makali sana yanayowezekana."

Kama njia ya mshikamano, Khatamy aliwaomba viongozi wengine wa Kiislamu kulaani shambulio hilo na kuungana na Wakenya wengine kwenda kuchangia damu. "Pia tunahubiri ujumbe wa upendo katika misikiti yetu na hata ya kuwa raia wanaofuata sheria na kuichukua dini yetu katika namna ya kuheshimika," alisema.

Wakati ukubwa wa mzozo huo ukiendelea kujulikana, wanasiasa wa Kenya walitumia vyombo vya habari vya kijamii kwa kutoa wito kwa wananchi kwenda kuchangia damu, ambayo inahitajika kwa vile mamia ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali kadhaa.

"Nimekuja hapa kuchangia damu kwa sababu hiki ndicho ninachoweza kufanya," alisema Nduati Ngethe, mwenye umri wa miaka 51, wakati akipanga foleni huko Kencom, moja ya vibanda vya kutoa damu mjini Nairobi.

"Mimi ni mchuuzi mnyonge, lakini vilio vya watoto wachanga ambao wangeweza kufa kwa kukosa damu kumenifanya nichukue hatua," alisema Nduati Ngethe .

"Shambulio hilo la kikatili limewaunganisha Wakenya bila ya kujali makabila, mbalimbali au dini zao," alisema Rose Mueni, mwenye umri wa miaka 25, mhudumu katika Creamy Inn kwenye maduka ya Westgate, akionesha mikono yake liliyochubuka baada ya kudondoka ngazini alipokuwa anakimbia. "Natumani kuwa tutaweza kutumia janga hili kama somo la kuwa wazalendo na wavumilivu wa maoni mbalimbali  kila mmoja na tofauti za kidini duniani.

Viongozi wa kidini walaani ugaidi

"Mashambulizi haya ya kusikitisha hayana uhusiano na dini yoyote," alisema Ally Ahmed, makamu mwenyekiti wa Msikiti wa Riadha ya Pumwani. "Hii kabisa ni kazi ya magaidi wenye uchu wa damu za watu na vikosi vyetu (vya Kenya) vinafanya kazi bila kuchoka kumaliza utekaji nyara huu na kuwaokoa mateka wasiokuwa na hatia."

"Sisi kama wahubiri na viongozi wengine wa Kiislamu tuko mstari wa mbele kuwapa muongozo kaka zetu wa Kiislamu dhidi ya imani kali," alisema Ally. "Kuua ni kinyume dhidi ya mafundisho ya Uislamu na ugaidi ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Watu hawapaswi kuua kwa sababu ya dini. Hakuna wa milele duniani, hivyo natuyafurahie maisha kama zawadi kutoka kwa Mungu bila ya kuwadhulumu wengine."

Abdullahi Abdi, mwenyekiti wa Jukwaa la Kitaifa la Viongozi wa Kiislamu, alisema kwamba ingawa magaidi walio kwenye jengo la Westgate wanadaiwa kuwa Waislamu, hilo haliwafanyi Waislamu wote kuwa magaidi.

"Sisi sote ni Wakenya wapenda amani," alisema Abdi Abdullahi.

"Hao waliouwa na kulemaza watu kwenye jengo la Westgate ni wahalifu na magaidi... sio Waislamu wa Kenya au Wakenya wa Kisomali," alisema Abdi. "Hivyo, tupendane na tusichochee uhasama wa kidini kwenye nchi hii nzuri."

"Wakristo na Waislamu wameishi kwa pamoja kwa salama kwa miaka nyingi nchini Kenya," alisema Askofu Joel Waweru wa Kanisa Anglikana nchini Kenya. "Hatupaswi kuwaruhusu magaidi kupandikiza mbegu ya chuki kwenye nyoyo zetu."

"Tumewaona maulamaa na viongozi wa Kiislamu wakijitokeza kuelezea bayana kwamba Waislamu na Uislamu hauhusiani kabisa na mauaji haya ya kikatili, mateso na uharibifu wa mali," alisema"Ningependa kuwatolea wito wanasiasa kutokutia mafuta kwenye cheche za uadui."

"Kuua watu wasiokuwa na hatia kama ilivyotokezea kwenye jengo la Westgate ni tendo la woga wa hali ya juu," alisema Sheikh Mohammed Khalifa, katibu wa Baraza la Maimamu na Wahadhiri la Kenya. "Nawatolea wito Wakenya wote kuungana kuwalaani wale wanaotenda matendo ya kigaidi dhidi ya watoto, wanawake na wanaume wasio hatia bila kujali dini zao."

"Katika Uislamu, kumwaga damu na kuharibu mali ni mambo yaliyoharamishwa kabisa. Kunaweza kuwa kichochea cha kuingia kwenye uhasama wa kidini na hilo litakuwa limekidhi maslahi ya magaidi, jambo ambalo sisi wahadhiri na maimamu lazima tuwe na hadhari nalo sana," alisema.

"Ningelipenda kaka na dada zetu wapenzi wasiokuwa Waislamu kujua kwamba Uislamu uko kwenye mambo matatu: imani kwa Mungu mmoja, huduma kwa umma, na mafundisho ya uvumilivu, haki na huruma," alisema Khalifa.

"Qur'an Tukufu inafunza kwamba yeyote anayemuua mwengine isipokuwa akiwa ameua au amefanya uhalifu, ni sawa na kwamba amewauwa wanadamu wote. Na yeyote anayenusuru maisha ya mtu mmoja ni kama aliyeokoa maisha ya watu wote."

"Kwa hivyo, Qur'an inatutolea wito wa kulinda utukufu wa maisha ya mwanadamu," alisema Khalifa.

Jibu la Somalia

Nchini Somalia, wafanyakazi na viongozi wa serikali pia waliyalaani mashambulizi hayo.

Sheikh Osman Ibrahim wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu aliyalaani mashambulizi hayo na kuyakana madai ya al-Shabaab kwamba Kenya inaupiga vita Uislamu au kuipiga vita Somalia.

"Kenya na Somalia hazipigani vita, ni majirani ambao wana maslahi ya pamoja ya kidiplomasia na kiuchumi, kwa hivyo mashambulizi hayo hayakuwa kwa maslahi ya Wasomali," alisema

"[Al-Shabaab] inamuita kila mtu kuwa si Muislamu ili kuhalalisha umwagaji damu," alisema Ibrahim. "Kila mtu anajua kuwa al-Shabaab haitetei dini yoyote ile."

Mbunge Dahir Amin Jesow alisema watu wa Somalia wako pamoja na Wakenya kwenye kipindi hiki kigumu.

"Tatizo la ugaidi linatuathiri na sisi hapa [Somalia] pia, hivyo lazima tupambane nao na tuuharibu,"

Ugaidi hauna mipaka ya kitaifa wala kikabila; ni kitisho kwa ubinadamu, alisema Jesow. Watu kote duniani lazima waungane kupambana na ugaidi kwa pamoja, alisema.

Qasim Moge Abdullahi, mkurugenzi wa Jumuiya ya Amani na Maendeleo ya Iniskoy, pia alilaani mashambulizi hayo, akiyaita ukikaji mkubwa dhidi ya Uislamu na haki za binadamu.

"Watu wanaouliwa na al-Shabaab ni raia wasio na silaha, ni wanawake na watoto, hivyo tunalaani kitendo hiki," alisema.

Abdullahi alisema nchi zinapaswa kushirikiana kuyaangamiza makundi kama al-Shabaab, lakini akaitolea wito serikali ya Kenya kutowalaumu watu wasiokuwa na hatia kwa matendo ya al-Shabaab na pia iwalinde Wasomali na Waislamu nchini Kenya dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi.


Usalama kwenye majengo yenye maduka waangaliwa upya.

"Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba tumepoteza maisha ya watu wengi na wale wote waliojeruhiwa," alisema Shah Noor, mmiliki wa duka la vifaa kwenye jumba hilo la maduka.

"Natamani kungelikuwa na namna ya serikali yetu kuweza kuepusha mashambulizi haya ya kigaidi,"  . "Biashara yangu na za wenzangu zitadorora kwa sababu watu watayahusisha majengo haya ya maduka na hatari na hivyo kujitenga kando."

Noor alisema Jumuiya ya Majengo ya Maduka Makubwa ya Kenya na serikali lazima wahakiki usalama wa majengo hayo mara moja.

Mbali na Wastegate, majengo mengine yenye maduka mengi jijini Nairobi ni Sarit Centre, The Village Market, Yaya Centre, Nakumatt Lifestyle, Thika Road Mall, Capital Centre, Galleria Shopping Mall, The Junction Mall na Prestige Plaza.

Baada ya mashambulizi kwenye jengo la Westgate, mengi ya majengo hayo yalifungwa kwa muda kama hatua ya tadhari kiusalama huku polisi wenye silaha wakipelekwa.

"Ni hatua ya muda ya kiusalama na jambo la busara kufanya kwenye hali iliyopo sasa, alisema Alfred Ng'ang'a, msemaji wa mtandao wa maduka makubwa ya Nakumatt, ambao unamiliki mengi miongoni mwa majengo hayo.

"Najua wateja hawatojisikia vizuri, lakini natarajia wanafahamu kuwa ni kwa ajili ya usalama wao wenyewe," alisema

Maduka mengi yalifunguliwa tena siku ya Jumatatu kwa muda maalum, huku oparesheni ya Westgate ukiendelea.

Wizara ya Usalama wa Ndani na Uratibu wa Serikali Kuu ya Kenya iliwaomba raia kukaa mbali na eneo la jengo la Westgate siku ya Jumatatu, kwani bado lilikuwa eneo la uhalifu. Wizara hiyo ilitoa nambari kadhaa za simu ambazo raia wanaweza kuulizia taarifa za jamaa na marafiki zao: 0202724154, 020310225, 0203226771, 0203532198 na 0203556780.

Poleni sana ndugu zetu wakenya:
Tupo pamoja katika wakati huu mgumu
Mchimba Riziki

Copyright © 2014. Mchimba Riziki- All Rights Reserved

Map

Live score